Pata taarifa kuu
UFARANSA-IS-MASHAMBULIZI-USALAMA

Taarifa za RFI juu ya ushiriki wa IS katika mashambulizi Isère

Jumanne Juni 30, Yassin Salhi alishtakiwa kwa mauaji kwa ushirikiano na kundi la kigaidi. Mashambulizi hayo " yanakwenda sambamba na itikadi ya Daech " kwa mujibu wa mwendesha mashtaka wa mji wa Paris.

Yassin Sahli, aliyehusika katika mauaji ya Ijumaa Juni 26, inasadikiwa kuwa alishinikizwa na IS kuendesha mashambulizi makali Ufaransa.
Yassin Sahli, aliyehusika katika mauaji ya Ijumaa Juni 26, inasadikiwa kuwa alishinikizwa na IS kuendesha mashambulizi makali Ufaransa. REUTERS/Emmanuel Foudrot
Matangazo ya kibiashara

François Molins amesema kuwa vitendo vya Yassin Salhi vinakwenda sambaba na "nia ya kigaidi ", hata kama anajaribu kujitetea akisema kwamba kitendo hicho "alikifanya kwa nia yake mwenyewe”.

Kulingana na vyombo vya sheria vya Ufaransa, Sahli Yassin aliweza kumtumia kwenye WhatsApp jamaa yake aliyejiunga na Islamic State picha yake, huku akishikilia kichwa cha mateka aliyemuua nchini Syria. Habari ambazo zilihibitishwa na vyanzo kadhaa vilivyowasiliana na RFI katika kundi hilo la Islamic State.

Kwa mujibu wa chanzo kimoja kilichowasiliana na RFI katika kundi la Islamic State, mashambulizi ya Ijumaa Juni 26 katika mji wa Isère yaliendeshwa kwa ushirikiano wa kundi la Kijihadi la Islamic State. Kwa upande mwingine, kwa mujibu wa mpiganaji mmoja nchini Syria kwa zaidi ya miaka miwili, mmoja wa wapiganaji wa Islamic State alimtaja mara kadhaa Saleh Yassin, kupitia mitandao ya kijamii na kwa njia ya simu, kuwa yuko tayari kuanzisha mashambulizi makali nchini Ufaransa.

Hata hivyo Yassin Salhi ameendelea kukanusha kuwa hakutumwa na kundi lolote au mtu yeyote kutekeleza mashambulizi hayo. Lakini kwa mujibu wa François Molins, mwendesha mashitaka wa mji wa Paris Paris, baadhi ya matukio hayasema uongo: kushikilia kichwa cha mateka aliyeuawa, mwili wa mwathirika uliyofungwa katika bendera ya kundi la Islamic State: " yote haya yanaonyesha kuwa kulikua na mkono wa Daech ", amesema François Molins.

Yassin Salhi aliendesha shambuliyo Ijumaa Juni 26 katika Kanisa moja lenye waumini kutoka jamii ya watu weusi katika mji wa Isère nchini Ufaransa. Watu tisa ikiwa ni pamoja na mchungaji mmoja waliuawa katika shambulio hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.