Pata taarifa kuu
UINGEREZA-EU-USHIRIKIANO

Ufaransa yatoa mapendekezo kwa kuizuia Uingereza kundoka katika EU

Ufaransa inataka mkataba ili kuzuia Uingereza kuondoka katika Umoja wa Ulaya lakini"bado kuna kazi" ya kufanya "hasa juu ya utawala wa uchumi," wasaidizi wa Rais François Hollande wamesema Jumatatu hii.

François Hollande akimpokea Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron katika Ikulu ya Elysée, Februari 15, 2016.
François Hollande akimpokea Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron katika Ikulu ya Elysée, Februari 15, 2016. MATTHIEU ALEXANDRE/AFP
Matangazo ya kibiashara

"Kuna dhamira ya kisiasa ya kuhitimisha" lakini "bado kuna kazi, hasa juu ya utawala wa uchumi", wasaidizi wa Rais wa Ufaransa wamebaini, baada ya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron katika Ikulu ya Elysée.

David Cameron na François Hollande hawakusema lolote baada ya mkutano huo wa kikazi uliotangazwa pamema asubuhi na ulidumu kwa karibu saa moja.

Uingereza inajadili suala la kuijiunga kwake kwa Umoja wa Ulaya na matumaini ya kufikia makubaliano katika mkutano wa Umoja wa Ulaya utakaofanyika Alhamisi na Ijumaa mjini Brussels, kabla ya kura ya maoni itakayoweza kufanyika mwishoni mwa msimu huu.

Hata hivyo, Ufaransa imetoa masharti manne, kukataa marekebisho yoyote ya mikataba ya Ulaya au kanuni za msingi za Muungano, Ulaya kwa ramani au kura ya turufu juu ya kupanuliwa kwa eneo la nchi zinazotumia sarafu ya Euro ambavyo vhuenda vikapingwa na nchi zisiokuwa katika eneo hili, kama vile Uingereza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.