Pata taarifa kuu
UINGEREZA-EU-USHIRIKIANO

Uingereza: Cameron atoa masharti yake kwa EU na kutishia kujiondoa

David Cameron ametishia Jumanne wiki hii nchi yake kujiondoa katika Umoja wa Ulaya iwapo hatapata mageuzi anayodai, kwa kuwasilisha madai yake kabla ya kura ya maoni ambayo anaona kama "Uamuzi wa maisha."

David Cameron wakati wa mkutano na Shirikisho la Viwanda nchini Uingereza, Novemba 9, 2015.
David Cameron wakati wa mkutano na Shirikisho la Viwanda nchini Uingereza, Novemba 9, 2015. REUTERS/Toby Melville
Matangazo ya kibiashara

Mara moja alijibu kwa kusema kuwa baadhi ya madai ni "matatizo mno", wakati ambapo Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema kuwa "sababu hizo ni za kijasiri" kuhusu makubaliano na London.

"Nina hakika kabisa kwamba tutapata makubaliano na Umoja wa Ulaya ambayo yatatakua sambamba na madai ya Uingereza", Waziri mkuu wa Uingereza amesema katika hotuba yake mbele ya vyombo vya habari. Vinginevyo "uanachama wetu utajadiliwa upya" kwa Umoja wa Ulaya, Cameron ameonya, huku akielezea kuwa hafuti "lolote" na kuwa nchi yake inaweza kuishi hata ikiwa nje ya Umoja wa Ulaya.

Cameron ameeleza kwa kina madai 4 ambayo alikua ameyazungumzia katika uamuzi wake, miaka mitatu iliyopita, kuandaa kura ya maoni kabla ya mwisho wa mwaka 2017. Mpango huu ulikuwa na lengo la kuwatuliza watu wanaounga mono Uingereza kujiunga na Ulaya kutoka kambi ya chama chake cha Consevative na kwa kukabiliana na maendeleo ya chama cha UKIP kinachopinga Uingereza kujiunga na Ulaya, mshindi wa uchaguzi wa Ulaya mwaka 2014.

Waziri mkuu wa Uingereza ameomba Umoja wa Ulaya kutambua kwamba Uingereza ni nchi yenye sarafu nyingi na haisababishi hasara kwa nchi ambazo si wanachama wa nchi zinazotumia sarafu ya Euro katika maamuzi yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.