Uingereza yakumbwa na mafuriko
Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron amewatembelea leo Jumatatu wakazi walioathirika na mafuriko kaskazini mwa Uingereza, mafuriko yaliotokana na mazingira ya hali isio kuwa ya kawaida, inayoathiri nchi kadhaa za Ulaya ya Magharibi.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Nchini Uhispania, joto kali lilio kwenye kiwango cha juu kuliko msimu wa wastani na kiwango cha chini cha mvua vimechangia kuondoka kwa majanga ya moto katika misitu.
Katika rasi ya Italia, shughuli kadhaa hususan magari yamepigwa marufuku kuingia barabarani katika miji mikubwa kadhaa kwa lengo la kupambana dhidi ya uchafuzi wa mazingira, unaosababishwa na kukosekana kwa mvua au upepo kwa muda wa wiki kadhaa.
Hali ambayo haijawahi kushuhudiwa kaskazini mwa Uingereza
Waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron, amekutana mapema Jumatatu hii asubuhi na askari waliokua wakishiriki katika zoezi la uokoaji na ulinzi wa majengo katika mji wa York, katika kaunti ya Yorkshire (kaskazini), kwa mujibu wa maneno alioandika katika akaunti yake binafsi ya twitter.
Katika mji huo wa kihistoria wa York, majengo 500 yamekumbwa na mafuriko na magari kadhaa yamepelekwa na maji.