UINGEREZA-UFARANSA-USHIRIKIANO
David Cameron ziarani Paris
Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron anazuru jijini Paris nchini Ufaransa kukutana na rais François Hollande.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Matangazo ya kibiashara
Ni ziara inayokuja baada ya Islamic State kushambulia jiji la Paris na kuwauwa watu zaidi ya 130 na wengine kujeruhiwa.
Viongozi hao watajdiliana kuhusu namna ya kuimarisha usalama katika ya mataifa yao na kwingineko barani Ulaya.
Tayari Uingereza imesema kuwa inatarajia kutumia zaidi ya Dola bilioni 18 nukta 2 kuimarisha Wizara ya ulinzi na kupambana dhidi ya ugaidi kwa muda wa miaka mitano ijayo.