Pata taarifa kuu
ULAYA-USAFIRI-UGAIDI

Baadhi ya viongozi waomba mabadiliko ya sheria ya usafiri Ulaya

Baada ya mafululizo wa mashambulizi ya hivi karibuni nchini Ufaransa, mataifa ya Ulaya yameanza kujidhatiti kwa kuchukua hatua ya kukabiliana na hali kama hiyo kuweza tena kutokea.

Reuters/Eric Gaillard
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa Baraza la Ulaya, Donald Tusk, amebaini kwamba kuna umuhimu wa kuwa makini na kuchukua hatua za kukabiliana na vitisho vya wanajihadi, huku mataifa yanayo jumuika katika eneo la Schengen kuweza kurekebisha baadhi ya Ibara za sheria za usafiri, ameendelea kusema, Donald Tusk.

Miongoni mwa maswali yaliyoulizwa mara nyingi, kuna yale kuhusu watu wanapewa uhuru wa kusafiri katika nchi za Umoja wa Ulaya. Kutokana na tishio la kigaidi, Umoja wa Ulaya umekua ukisita kati ya usalama na nia ya kuzingatia uhuru wa watu.

Nchi kadhaa, ikiwa ni pamoja na serikali ya Uhispania, hazifichi matakwa yao ya kudhibitiwa kwa matumizi ya mkataba wa Schengen, au kujadili hilo. Hata hivyo jambo hilo ni moja ya mafanikio ya msingi ya wananchi wa Ulaya: kuwa na uwezo wa kusafiri bila mipaka.

Serikali nyingi pia zinataka Bunge la Ulaya kutoa haraka rasimu ya agizo inayoitwa "PNR" kwa " jina la kila msafiri anapovuka mpaka wa nchi moja kuingia nchi nyingine".

Mfumo huu utayalazimu mashirika ya ndege yanayofanya safari zao barani Ulaya kutoa taarifa kwa polisi na Idara za upelelezi za nchi wanachama kuhusu abiria wanaoingia na kutoka katika nchi za bara la Ulaya. Lakini Bunge ambalo limekua likijikita katika ulinzi wa uhuru wa raia, halikubaliane na mfumo huo. Bunge hilo limetoa hoja kadhaa kuhusiana na utaratibu huo.

Kwa Mbunge wa Umoja wa Ulaya kutoka Uholanzi Sophie In't Veld, makamu mwenyekiti wa kundi la Wabunge kutoa vyama vya Kiliberali, hakuna uhusiano kati ya mashambulizi yaliyotokea nchini Ufaransa na kukosekana kwa mfumo wa PNR. "Hakuna uhusiano wowote! ", amesema akielezea mshangao wake, Sophie In't Veld.

" Wiki iliyopita, kama karibu mashambulizi yote makubwa, magaidi huwa wakijulikana na Idara za usalama. Kupata data za abiria, hakuwezi kubadili chochote, ikiwa ni pamoja na Ufaransa, ambayo tayari ina uwezekano wa kukusanya data za PNR, mimi sioni tatizo?", amesema Sophie In't Veld.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.