Pata taarifa kuu
UFARANSA-UGAIDI-IS

Polisi yaendelea na msako dhidi ya watuhumiwa wawili

Maelfu ya askari wamepelekwa kwenye maeneo ambayo watuhumiwa wawili wa shambulio la jijini Paris katika ofisi za jarida la Charlie Hebdo wamekimbilia, huku wakifanya msako wa nyumba kwa nyumba.

Vikosi vya usalama vinaendelea na operesheni ya kuwasaka watuhumiwa wawili ambao ni ndugu wanaoshukiwa kuhusika katika mauaji ya watu 12 na shambulio dhidi ya jarida la vibonzo la Charlie Hebdo, Januari 7 mwaka 2015.
Vikosi vya usalama vinaendelea na operesheni ya kuwasaka watuhumiwa wawili ambao ni ndugu wanaoshukiwa kuhusika katika mauaji ya watu 12 na shambulio dhidi ya jarida la vibonzo la Charlie Hebdo, Januari 7 mwaka 2015. REUTERS/Pascal Rossignol
Matangazo ya kibiashara

Msako unafanyika wakati huu ambapo mkuu wa shirika la ujasusi nchini Uingereza, ameonya kuwa huenda wapiganaji wa kiislamu wamepanga kufanya shambulio jingine kwenye nchi za Magharibi.

Shambulio hili limewaleta pamoja wanasiasa nchini Ufaransa ambapo siku ya Alhamisi rais Francois Hollande alikutana kwa mazungumzo na rais wa zamani wa nchi hiyo, Nicolas Sarkozy ambaye amesema ni lazima Wafaransa waungane dhidi ya magaidi.

Kwa upande wao wachoraji wa vibonzo duniani kote wameungana na kusisitiza kuendelea kutoa maoni yao kupitia vibonzo bila uoga huku wengine wakitaka elimu kutolewa zaidi kuelewa taaluma hiyo kama.

Watu 12 waliuawa kwenye shambulio la Juma hili ambapo watu wawili wenye silaha walivamia ofisi za jarida la Charlie Hebdo na kuanza kuwafyatulia risasi wafanyakazi wake na polisi.

Zaidi ya askari polisi elfu themanini waanaendelea na operesheni ya kuwasaka watuhumiwa wawili ambao ni ndugu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.