Pata taarifa kuu
AFRIKA-UFARANSA-SHAMBULIO-UGAIDI

Shambulio dhidi ya Charlie Hebdo: vyombo vya habari duniani vyalani

Shambulio la kigaidi dhidi ya jarida la vibonzo la Charlie Hebdo limewagusa watu kutoka jamii mbalimbali hususan jamii ya waandishi wa habari nchini Ufaransa, lakini pia barani Afrika na kwingineko duniani.

Mchoraji Vibonzo Charb, mhariri wa jarida la vibonzo la "Charlie Hebdo" katika makao makuu ya jarida hilo, mwezi  Septemba mwak 2012.
Mchoraji Vibonzo Charb, mhariri wa jarida la vibonzo la "Charlie Hebdo" katika makao makuu ya jarida hilo, mwezi Septemba mwak 2012. REUTERS/Jacky Naegelen/Files
Matangazo ya kibiashara

Watu kumi na wawili, ikiwa ni pamoja na wabunifu maarufu Cabu, Wolinski, Tignous na Charb pamoja na askari wawili, waliuawa.

Hisia tofauti kufuatia tukio hilo zimekua zikitolewa nchini Algeria, Côte d’Ivoire na Mauritania. Taarifa za kulani tukio hilo zimekua zikitolewa duniani kote, bila kusahau vyombo vya habari barani Afrika, ambavyo vinabaini kwamba tukio hilo ni pigo kubwa kwao na kwa raia kutoka nchi mbalimbali duniani.

Algeria : « pigo kubwa kwa jamii ya wanahabari »

Nchini Algeria, hisia tofauti zimekua zikitolewa katika jumba la mikutano la waandisi wa habari, ambalo lilikabiliwa na vitendo vya ugaidi katika miaka iliyopita.

Machozi yamekua yakiwatiririka waandishi wa habari katika mataifa kadhaa barani Afrika baada ya shambulio hilo dhidi ya jarida la vibonzo la Charlie Hebdo.

Mmoja ya wachoraji katuni ambao wanafanya kazi katika majengo hayo yaliyoshambuliwa ameeleza kwamba haelewi kuona mwaka 2015 watu wanauawa kwa ajili ya kuchora aidha maoni.

Katika mwaka 1990, waandishi wa habari 117 na wafanyakazi wa vyombo vya habari waliuawa nchini Algeria. Wakati huo mashambulizi mawili yakutisha yaliendeshwa dhidi ya vyombo vya habari vya taifa. Mwaka 1994, kundi la watu wenye silaha waliingia ndani ya chumba cha habari cha jarida la Hebdo Libéré na kuwafyatulia risase wafanyakazi. Watu wawili waliuawa katika shambulio hilo. Mwaka 1996, bomu lililotegwa ndani ya gari lilipuka kando kidogo na jarida moja mjini Algiers, na kusababisha vifo vya watu tisa.

Masikitiko makubwa Mauritania

Nchini Jamhuri ya Kiislamu ya Mauritania, waandishi wa habari wengi wameghadhabishwa na shambulio dhidi ya jarida la vibonzo la Charlie Hebdo, na kusema kuwa hawatakubali haki zao ziendeleye kukandamizwa.

Akihojiwa na RFI, Moussa Ould Samba Sy, mwenyekiti wa Umoja wa vyombo vya habari binafsi nchini Mauritania, amesema kuwa ana hofu ya kutokea kwa visa kama hivyo katika jamii ya wanahabari, huku akilaani wale ambao wanachukulia kama mzaha kwa kile kilichotokea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.