Pata taarifa kuu
Ufaransa yaomboleza vifo vya watu 12 waliouawa mjini Paris

Vyombo vya Habari nchini Ufaransa Vyashirikiana pamoja, Katika kuomboleza.

Wakati wananchi wa Ufaransa wanaomboleza Vifo vya watu kumi na wawili waliouawa katika shambulizi lililolenga ofisi za jarida la vibonzo la kila wiki la Charlie Hebdo Hapo Jana, waandishi wa habari mjini Paris wameonyesha mshikamano kwa waandishi wa habari wa jarida hilo la Vibonzo katika kile walichokiita:” Je suis Charlie” yaani Mimi ni Charlie.

Matangazo ya kibiashara

Tangazo lililosomwa na mkuu wa radio ya kimataifa ya Ufaransa, RFI Cecile Megie baada ya kumalizika kwa mkutano wa waandishi wote wa habari lilianza na matamshi ya kifaransa yanayosema: "Mimi ni Charlie",

na haya ndio matamshi ya wandishi wote kama inavyoainishwa katika tangazo hilo:
Jana mjini Paris nchini Ufaransa ofisi za jarida la vibonzo la kila wiki la Charlie Hebdo lilishambuliwa na watu wenye silaha, wanaosadikiwa kuwa ni magaidi.

Watu kumi na wawili waliuawa : wakiwemo waandishi wa habari, polisi na marafiki.
Kwa niaba ya vyombo vya habari vya Ufaransa, mawazo yetu yanaelekezwa kwa wanahabari wenzetu waliokufa, na rambirambi zetu ziende kwa familia za wafanyakazi wote wa jarida hilo la vibonzo, waandishi wa habari wote, nchini Ufaransa;

Kifo cha waandishi hawa kimedhihirisha kuwa uhuru wa kujieleza na ule wa kuutuma ujumbe kwa njia ya vibonzo, uko hatarini. Dhamiri za wengi zimesamabaratika wakati huu.

Jarida la vibonzo liligusa hisia za watu wengi, lakini pia liliamsha dhamiri za wengi. Lahamasisha kuepuka ubaguzi na kuwa na kuachana na msimamo mkali.

Ambao waliuawa jana walikuwa wenye kutuchekesha na hivyo kutuweka katika hali ya uhuru.

Uhuru wa mawazo na uhuru wa kujieleza ndio vigezo vya kazi yetu ya kila siku.
Katika siku hii ya maombolezo, tunatumia fursa hii kuhakikisha kuwa hatutakubali vitisho wala kuhofiwa maisha kwa vyovyote vile.Hatutanyamaa kimya, nasi tutapiga vita kila aina ya ubaguzi.

Vyombo vyote vya habari vya Ufaransa vimejipanga kwa hali na mali kuhakikisha jarida la vibonzo Charlie Hebdo linaendelea kuishi.

Sote kwa pamoja tumeshirikiana ili kutetea uhuru wa vyombo vya Habari. Na tutaendelea kuutetea kwa niaba yao.

Waliosahini Tangazo hilo:

Christopher Baldelli (RTL), Christophe Barbier (L'Express), Jean-Paul Baudecroux (NRJ), Pierre Bellanger (SKYROCK), Jérôme Bellay (Le Journal du Dimanche), Nicolas Beytout (L’Opinion), Véronique Cayla (ARTE), Matthieu Croissandeau (L’Obs), Nicolas de Tavernost (M6), Bruno Delport (Nova), Louis Dreyfus (Le Monde), Marc Feuillée (Le Figaro), Mathieu Gallet (Radio France), Etienne Gernelle (Le Point), Emmanuel Hoog (AFP), Jean Hornain (Le Parisien),Patrick Le Hyaric (L'Humanité), Gérard Leclerc (LCP-AN), Gilles Leclerc (Public Sénat), Bertrand Meheut (CANAL+), Francis Morel (Les Echos), Denis Olivennes (Lagardère Active / Europe 1), Nonce Paolini (TF1), Fabienne Pascaud (Télérama), Rémy Pflimlin (France Télévisions), Matthieu Pigasse (Les Inrockuptibles), Dominique Quinio (La Croix), Olivier Royant (Paris Match), Marie-Christine Saragosse (France Médias Monde), Jean-Christophe Tortora (La Tribune), Jean-Eric Valli (Les Indés Radio), Maurice Szafran (Le Magazine Littéraire), Alain Weill (NextRadioTV)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.