Pata taarifa kuu
UFARANSA-USALaMA

Milio ya risasi yasikika kusini mwa Paris

Milio ya risasi imesikika Alhamisi Januari 8 mapema asubuhi pembezoni mwa kitongoji kimoja kusini mwa mji wa Paris, kwenye mpaka kati ya Malakoff na Montrouge.

Maafisa wa Idara za dharura na vikosi vya usalama katika eneo la tukio katika kitongoji cha Montrouge (kusini mwa Paris), Alhamisi Januari 8 mwaka 2015.
Maafisa wa Idara za dharura na vikosi vya usalama katika eneo la tukio katika kitongoji cha Montrouge (kusini mwa Paris), Alhamisi Januari 8 mwaka 2015. AFP/Thomas Samson
Matangazo ya kibiashara

Mtu mmoja ambaye alikua akivalia fulana inayozuia risase kuingia muilini, akiwa na bunduki alimfyatulia risasi askari polisi wa kitongoji hicho pamoja na afisa wa barabara. Wawili hao wako katika hali maututi.

Waziri wa mambo ya ndani, Bernard Cazeneuve, ameondoka ghafla katika mkutano wa baraza la mawaziri uliokua ukifanyika Ikulu, na kujielekeza eneo la tukio. Waziri Cazeneuve, ameeleza kwamba mtu huyo aliye husika na kitendo hicho alitimka.

Alipowasili mapema asubuhi kwenye eneo la tukio mwandishi wa RFI, Carrie Nooten, alipata mashuhuda wengi, ambao walimuelezea mkasa huo. Kwa mujibu wa Carrie Nooten, “ chanzo cha tukio hilo ni ajali iliyotokea kwenye barabara kuu inayoelekea Paris. Maafisa wa jiji waliingilia kati. Wakati huo pembezoni mwa eneo hilo kulikotokea ajali hiyo, alionekana mtu akibebelea kifurushi chake mgongoni, ambaye alifyatua risasi mbili". Kwa mujibu wa mashahidi, askari polisi waliyokua eneo hilo walilazimika kufyatua nao pia risasi ili waweze kumkagua na kumkamata mtu huyo aliyefyatua risase kwa mara ya kwanza.

Muhalifu huyo aliendelea kufyatua risasi, na baadaye kuwafyatulia risasi askari polisi mmoja na afisa wa barabara, ambao wako katika hali ya maututi.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Ufaransa AFP, mshukiwa alikamatwa kwenye eneo la tukio.

Lakini alipowasili kwenye eneo la tukio, Waziri wa mambo ya ndani, Bernard Cazeneuve, amebaini kwamba mtu aliye husika na kitendo hicho alitimka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.