Pata taarifa kuu
UFARANSA-UGAIDI-IS

Watekaji nyara wauawa Dammartin-en-Goële

Baada ya shambulio dhidi ya jarida la vibonzo la kila wiki la Charlie Hebdo, ambalo liligharimu maisha ya watu 12 Jumatano, Januari 7, polisi walivamia kiwanda cha uchapishaji ambapo watuhumiwa wakuu wawili ameaminika wamejificha katika kitongoji cha Dammartin-katika-Goële , kilomita 40 kaskazini ya mji wa Paris.

Makomando wa Ufaransa wakianzisha mashambulizi katika kitongoji cha Dammartin-en-Goële.
Makomando wa Ufaransa wakianzisha mashambulizi katika kitongoji cha Dammartin-en-Goële. AFP PHOTO / JOEL SAGET
Matangazo ya kibiashara

Ndugu wawili wameuawa. Mateka ameondolewa ndani ya kiwanda hicho akiwa salama. Askari wa kikosi maalum cha GIGN amejeruhiwa.

■ Chérif et Saïd Kouachi wameuawa wakati vikosi vya usalama vilipovamia na kuanzisha mashambulizi katika kitongoji cha Dammartin-en-Goële. Mateka ameokolewa akiwa salama. Kwa sasa operesheni ya vikosi vya usalama imemalizika.

Mtu mmoja amekua ametakwa nyara katika kitongoji cha Dammartin-en-Goële, katika mji wa Seine-et-Marne.
Mtu mmoja amekua ametakwa nyara katika kitongoji cha Dammartin-en-Goële, katika mji wa Seine-et-Marne. REUTERS/Eric Gaillard

■ Utafiti. Ijumaa asubuhi, kulikuwepo na ubadilishanaji wa risasi kati ya polisi na watu wanaoshukiwa kuwa watuhumiwa hao wawili ambao ni ndugu kwenye barabara kuu inayojulikana kwa jina la National 2. Wawili hao walipenya na kuvamia kiwanda cha kuchapisha magazeti cha Dammartin-en-Goële, katika mji wa Seine-et-Marne wakiwa na mateka mmoja.

■ Uchunguzi. Wakati huo huo, uchunguzi unaendelea. Watu tisa ambao ni ndugu au jamaa za watuhumiwa hao waliohusika katika mauaji ya watu 12 kwenye makao makuu ya jarida la vibonzo la kila wiki la Charlie Hebdo wamewekwa chini ya ulinzi. Hata hivyo uchunguzi umeanziahwa kuhusu "uhusiano" kati ya watuhumiwa hao wawili ndugu na mtu aliyefyatua risasi na kuwajeruhi watu kadhaa akiwemo askari polisi, ambaye baadaye alifariki kutokana na majeraha katika kitongoji cha Montrouge.

Wakati operesheni ya vikosi vya usalama ikianza katika kitongoji cha Dammartin-en-Goële ili kwadhibiti watekaji nyara,ambao wameaminika kuwa ni ndugu wawili waliohusika katika shambulio la jarida la vibonzo la Charlie Hebdo.
Wakati operesheni ya vikosi vya usalama ikianza katika kitongoji cha Dammartin-en-Goële ili kwadhibiti watekaji nyara,ambao wameaminika kuwa ni ndugu wawili waliohusika katika shambulio la jarida la vibonzo la Charlie Hebdo. AFP PHOTO / JOEL SAGET

■ Maandamano ya kitaifa. Jumapili Januari 11, maandamano ya kitaifa yatafanyika katika miji mbalimbali, maandamano ambayo yaliitishwa na vyama vikuu vya Republican vyama vya wafanyakazi, taasisi mbalimbali na jumuiya ya Waislam nchini Ufaransa. Lakini umoja wa kitaifa iliotangazwa umeonekana kuingilia na mgawanyiko, Marine Le Pen amelani kuona chama cha Front National kinapigwa marufuku kushiriki katika maandamano hayo.

Wanafunzi wa shule moja katika kitongoji cha Dammartin-en-Goële,kaskazini mashariki mwa Paris wakiondolewa na vikosi vya usalama, Ijumaa Januari 9 mwaka 2015.
Wanafunzi wa shule moja katika kitongoji cha Dammartin-en-Goële,kaskazini mashariki mwa Paris wakiondolewa na vikosi vya usalama, Ijumaa Januari 9 mwaka 2015. AFP PHOTO / DOMINIQUE FAGET

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.