Pata taarifa kuu
BRAZIL-MICHEZO YA OLIMPIKI

Michezo ya Olimpiki yafikia tamati

Michezo ya Olimpiki ambayo imekuwa ikifanyika nchini Brazil imemalizika usiku wa kuamkia leo baada ya kufanyika kwa tamasha la kuvutia katika uwanja wa Maracana jijini Rio de Janeiro.

Tamasha la kuvutia lafanyika katika uwanja wa Maracana katika kumalizia michezo ya Olimpiki jijini Rio de Janeiro.
Tamasha la kuvutia lafanyika katika uwanja wa Maracana katika kumalizia michezo ya Olimpiki jijini Rio de Janeiro. REUTERS/Stoyan Nenov
Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya wanamichezo elfu 11 kutoka Mataifa 207 walishiriki katika Michezo hiyo ambayo ilifanyika majira ya joto.

Kwa mara ya kwanza nchi za Kosovo na Sudan Kusini zilishiriki, lakini pia kuliwa na wachezaji ambao waliwakilisha wakimbizi duniani ambao pia walishriki katika michezo mbalimbali.

Kulikuwa na Micehezo 28 katika mashindano haya ikiwemo kwa mara ya kwanza raga kwa wachezaji saba kila upande na mchezo wa Golf.

Marekani imeubuka mabingwa duniani kwa kumaliza michezo hii kwa kupata medali 122, zikiwemo 46 za dhahabu.

Uingereza imemaliza ya pili kwa medali 67, China imechukua nafasi ya tatu, Urusi ya nne na Ujerumani ya tano.

Wenyeji Brazil walimaliza katika nafasi ya 13 kwa medali 19, zikiemo saba za dhabu.

Kenya imeendelea kufanya vizuri kwa kumaliza katika nafasi ya 15 duniani na kuongoza barani Afrika kwa medali 13, Sita za dhahabu, Sita za fedha na moja ya shaba.

Licha ya kuwepo kwa mpangilio mbaya wa usafiri kwa baadhi ya wanariadha, Kenya imefanya vizuri katika michezo hii ya Olimpiki ukilinganisha na mambo yalivyokuwa wakati wa Michezo ya Olimpiki jijini London mwaka 2012.

Eliud Kipchoge siku ya kwisho ya michezo hii aliishindia Kenya medali ya dhahabu katika mbio za Marthon kwa upande wanaume, lakini wanaraidha wengine watakaokumbukwa ni Usain Bolt kutoka Jamaica ambaye akitetea mataji yake katika mbio za Mita 100, 200 na zile za kupokezana kijiti Mita 400 na anastaafu riadhaa.

Wapenzi wa riadha pia hawatamsahau Mo Farah, mwanariadha wa Uingereza ambaye ametetea mataji ya mbio za Mita 5000 na 10 000.

Michezo ijayo itafanyika mwaka 2020 jijini Tokyo Japan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.