Pata taarifa kuu
OLIMPIKI-BRAZIL 2016-RIADHA

Mather Centrowitz ashinda mbio za Mita 1500, Mo Farah aweka rekodi mbio za Mita 5000

Mmarekani, Mather Centrowitz ameishindia nchi yale medali ya dhahabu katiia mbio za Mita 1500 kwa upande wa wanaume katika Michezo ya Olimpiki nchini Brazil.

Mather Centrowitz akisherehekea ushindi wa mbio za Mita 1500 Michezo ya Olimpiki Agosti 21 2016 nchini Brazil
Mather Centrowitz akisherehekea ushindi wa mbio za Mita 1500 Michezo ya Olimpiki Agosti 21 2016 nchini Brazil Olympic Games 2016
Matangazo ya kibiashara

Centrowitz mwenye umri wa miaka 26 alimaliza mbio hizo mwa muda wa dakika 3 sekunde 50 nukta 00.

Taoufik Makhloufi kutoka Algeria bingwa wa mwaka 2012 wakati Michezo ilipofanyika jijini London nchini Uingereza alishindwa kutetea taji lake na kumaliza wa pili na kujinyakulia medali ya fedha kwa muda wa dakika 3 sekunde 30 nukta 11.

Nick Willis kutoka New Zealand naye alipambana na kumaliza katika nafasi ya tatu kwa muda wa dakika 3 na sekunde 50 nukta 24.

Bingwa wa mwaka 2008 Asbel Kiprop kutoka Kenya ambaye anafahamika kwa kuanza wa mwisho na baadaye kuwapita wenzake, alishindwa kuonesha ubabe wake baada ya kumaliza katika nafasi ya sita kwa muda wa dakika 3 sekunde 50 nukta 87.

Mo Farah mwanariadha wa Uingereza akisherehekea ushindi wa mbio za Mita 5000 Michezo ya Olimpiki Brazil 2016
Mo Farah mwanariadha wa Uingereza akisherehekea ushindi wa mbio za Mita 5000 Michezo ya Olimpiki Brazil 2016 Olmpic Games

Katika mbio za Mita 5000 kwa upande wa wanaume, Mo Farah kutoka Uingereza alifanikiwa kutetea taji lake aliloshinda mwaka 2012 jijini London kwa kumaliza kwa muda wa dakika 13 sekunde 3 nukta 30.

Farah mwenye umri wa miaka 33, aliyezaliwa nchini Somalia lakini ni raia wa Uingereza ameingia katika vitabu vya historia kwa kuwa mwanariadha bora wa nchi hiyo kushinda medali ya dhahabu katika mbio za Mita 5000 na 10000 wakati wa Michezo ya Olimpiki mwaka 2012 na 2016.

Nafasi ya pili ilimwendea Paul Kipkemoi Chelimo raia wa Marekani lakini mzaliwa wa Kenya, aliyemaliza kwa muda wa dakika 13 sekunde 3 nukta 90.

Hagos Gebrhiwet kutoka Ethiopia alishinda medali ya shaba kwa kumaliza kwa dakika 13 sekunde 04 nukta 35.

Kwa mara ya kwanza, wanariadha wa Kenya walishindwa kufuzu katika fainali ya mbio hizi za Mita 5000 katika Michezo hii ya Olimpiki.

Marekani inaendelea kuongoza jedwali ya medali kwa medali 116, zikiwemo 43 za dhahabu.

Uingereza ni ya pili kwa medali 66, China ya tatu kwa medali 70, Urusi ya nne kwa medali 53, Ujerumani ya tano kwa medali 41 huku Kenya ikiwa ya 16 duniani na ya kwanza barani Afrika kwa medali 12 zikiwemo 5 za dhahabu, 6 za fedha na moja ya shaba.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.