Pata taarifa kuu
OLIMPIKI-BRAZIL 2016-RIADHA

Eliud Kipchoge aishindia Kenya medali ya dhahabu katika mbio za Marathon

Mkenya Eliud Kipchoge ameshinda medali ya dhahabu katika mbio za Marathon kwa upande wa wanaume katika siku ya mwisho ya Michezo ya Olimpiki siku ya Jumapili nchini Brazil.

Eliud Kipchoge  akisherehekea ushindi wa mbio za Marathon Michezo ya Olimpiki nchini Brazil Agosti 21 2016
Eliud Kipchoge akisherehekea ushindi wa mbio za Marathon Michezo ya Olimpiki nchini Brazil Agosti 21 2016 Olympic Games 2016
Matangazo ya kibiashara

Kipchoge mwenye umri wa miaka 31, alishinda mbio hizo kwa muda wa saa 2 dakika 8 na sekunde 44.

Kuelekea katika Michezo hii, Kipchoge amekuwa akishiriki katika mbio za Chicago Marathon, London Marathon na Berlin Marathon na kumaliza katika nafasi ya kwanza.

Mwaka 2008 katika Michezo ya Olimpiki iliyofanyika jijini Beijing nchini China, alishiriki mbio za Mita 5000 na kumaliza wa pili na mwaka 2004 jijini Athens nchini Ugiriki alimaliza katika nafasi ya tatu.

Ushindi huu unatimiza ndoto yake ya kushinda medali ya dhahabu katika mashindano makubwa kama Marathon baada ya kushiriki kwa muda mrefu.

Nafasi ya pili ilimwendea Mwiethiopia, Feyisa Lilesa huku Galen Rupp akiishindia Marekani medali ya shaba kwa kumaliza wa tatu.

Kenya imemaliza Michezo hii kwa medali 13, sita za dhahabu zingine sita za fedha na moja ya shaba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.