Pata taarifa kuu
IRAQ-SIASA

Matokeo ya uchaguzi kutangazwa kwa muda wowote nchini Iraq

Wananchi wa Iraq wanasubiri matokeo ya Uchaguzi wa wabunge uliofanyika jana, mwaka mmoja kabla ya tarehe iliyokuwa imepangwa kufuatia maandamano makubwa dhidi ya serikali.

Mpiga kura huko Baghdad, kwa uchaguzi wa wabunge Jumapili, Oktoba 10, 2021.
Mpiga kura huko Baghdad, kwa uchaguzi wa wabunge Jumapili, Oktoba 10, 2021. AFP - AHMAD AL-RUBAYE
Matangazo ya kibiashara

Wapiga kura Milioni 25 waliandikishwa kushiriki kwenye Uchaguzi huo, lakini ripoti zinseema kuwa, ni idadi ndogo ya wapiga kuwa, ndio waliojitikeza wengi wakiwa wazee, huku vijana wakisusia Uchaguzi huo.

Ni asilimia 30 ya wapiga kura ndio waliojitokeza kushiriki kwenye Uchaguzi huu, ikiw ani idadi ndogo kuwahi kushuhudiwa katika historia ya uchaguzi nchini humlo, ikilinganiushwa na asilimia 44.5 iliyojitokeza mwaka 2018.

Vijana wengi waliosalia nyumbani badala ya kwenda kupiga kura, wanadai kuwa imani kwa wanasiasa nchini humo imepungua kufuatia ripoti  za mara ufisadi na ukosefu wa ajira.

Mpaka sasa haijabainika ni chama kipi kitaibuka mshindi, lakini wadadidi wa siasa za Iraq wanaona kuwa huenda Waziri Mkuu wa sasa Mustafa al-Kadhemi akashindwa kwenye Uchaguzi huu.

Wagombea 3,200 kutoka vyama 167 wanawania nafasi  329 katika bunge la nchi hiyp na baada ya matokeo, kutakuwa na mazungumzo kuhusu ni nani awe rais, Waziri Mkuu na Mawaziri.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.