Pata taarifa kuu
Marekani - Usalama - Iraq

Wanajeshi wa Marekani watekeleza mashambulizi anga nchini Iraq

Jeshi la Marekani limetekeleza mashambulizi ya angaa dhidi ya makundi ya wapiganaji yanayoungwa mkono na serikali ya Iran, nchini Iraq Na Syria, baada kushambuliwa kwa kambi ya Marekani nchini Iraq.

wanajeshi wa Marekani nchini Iraq
wanajeshi wa Marekani nchini Iraq © afp
Matangazo ya kibiashara

Taarifa ya jeshi la Marekani, imeeleza kuwa, mashambulizi hayo yamelenga maghala mawili ya kuhifadhi silaha yanayotumiwa na wapiganaji hao nchini Syria na moja nchini Iraq.

Marekani haijasema iwapo mashambulizi hayo yamesababisha maafa au majeruhi lakini, Shirika la Haki za Binadamu la Uingereza linasema wapiganaji watano wameauwa na wengine wamejeruhiwa.

Nalo Shirika la Habari la Syria, SANA, limesema mtoto mmoja ameauwa katika mashambulizi hayo na wengine watatu wamejeruhiwa.

Hatua hii imekuja baada ya maagizo ya rais Joe Biden ambaye hii ndio mara ya pili anaagiza kushambuliwa kwa wapiganaji wanaoungwa mkono na Iran.

Tangu kuanza kwa mwaka 2021, kumekuwa na mashambulizi 40 dhidi ya maeneo yenye maslahi ya Marekani nchini Iraq, nchi ambayo ina wanajeshi wan chi hiyo 2,500 kupambana na kundi la Islamic State.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.