Pata taarifa kuu
IRAQ-USALAMA

Watu zaidi ya 50 wafariki baada ya moto kuzuka katika hospitali ya Al-Hussein

Wagonjwa zaidi ya 50 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 22 wamejeruhiwa baada ya moto kuzuka katika wodi ya wagonjwa wa Corona katika Hospitali ya Al-Hussein katika mji wa Nasiriya, kusini mwa Iraq, msemaji wa maafisa wa afya ameliambia shirika la habari la AFP.

Watu wakiangalia uharibifu uliosababishwa na moto uliozuka katika wodi ya wagonjwa wa Corona katika hospitali ya al-Hussain, huko Nassiriya, Iraq, Julai 13, 2021.
Watu wakiangalia uharibifu uliosababishwa na moto uliozuka katika wodi ya wagonjwa wa Corona katika hospitali ya al-Hussain, huko Nassiriya, Iraq, Julai 13, 2021. REUTERS - KHALID AL-MOUSILY
Matangazo ya kibiashara

Sababu ya moto haijulikani, lakini ripoti za mwanzo zinaonyesha kuwa ulianza baada ya tenki ya oksijeni kulipuka.

"Waathiriwa wamefariki dunia baada ya miili yao kuteketea kwa moto na shughuli ya kutafuta miili mingine inaendelea," amesema Haydar al-Zamili, akiongeza kuwa wodi hiyo ilikuwa na vitanda 60. Moto bado ulikuwa ukiendelea usiku kucha , kulingana na mwandishi wa shirika la habari la AFP.

Wakati huo huo Waziri Mkuu wa Iraq Mustafa al-Kadhemi ameagiza kukamatwa kwa mkuu wa hospitali.

Spika wa bunge la Iraq Mohamed al-Halbousi ameandika kwenye ukurasa wake wa  twitter akisema kwamba kisa hicho cha moto katika hospitali hiyo ni dhibitisho tosha la kushindwa kuwajibika katika majukumu ya kulinda maisha ya waIraqi, na ni wakati wa kukomesha janga hili".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.