Pata taarifa kuu
IRAQ-SIASA

Iraq yafanya Uchaguzi wa wabunge chini ya ulinzi mkali

Uchaguzi wa mapema wa wabunge unafanyika Jumapili hii nchini Iraq, miaka miwili baada ya maandamano makubwa ya vijana mitaani ambao walidai mabadiliko, kukomeshwa kwa ufisadi, ajira, huduma bora za umma. Maandamano ambayo yalikandamizwa sana.

Dans un bureau de vote à Bagdad le 10 octobre 2021.
Dans un bureau de vote à Bagdad le 10 octobre 2021. AFP - SABAH ARAR
Matangazo ya kibiashara

Oktoba 10, Wairaq milioni 25 wametakiwa kupiga kura kuwachaguwa wabunge 329. Uchaguzi ambao unafanyika chini ya ulinzi mkali.

Tuko katika shule ambayo inashikilia vituo kadhaa vya kupigia kura katika kitongoji cha Al Sadoun katikati mwa Baghdad. Na kufikia shule hii, ilikuwa ni lazima kupitisha kamba za usalama, kutafutwa.

Makumi ya maafisa wa polisi wameonekana wakitoa ulinzi mkali kwenye vituo vya kupigia kura katika eneo la Al Sadoun katikati mwa Baghdad.

Usalama umeimarishwa kwa sababu ya hofu ya mashambulio katika nchi hii isiyo na utulivu, ambayo inakabiliwa na mashambulio ya kundi la Islamic State  na machafuko ya wanamgambo wenye silaha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.