Pata taarifa kuu
MAREKANI

Shambulio la uwanja wa ndege wa Kabul: Biden aahidi kulipiza kisasi dhidi ya IS

Rais wa Marekani Joe Biden katika hotuba yake kwa taifa, amesema kuwa zoezi la kuondoa raia wakigeni kutoka Afghanistan itaendelea licha ya shambulio lililogharimu maisha ya watu kadhaa, hususan wanajeshi 13 wa Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Kabul, nchini Afghanistan.

Rais wa Marekani Joe Biden wakati wa hotuba yake kuhusu Afghanistan katika Ikulu ya White House Agosti 26.,
Rais wa Marekani Joe Biden wakati wa hotuba yake kuhusu Afghanistan katika Ikulu ya White House Agosti 26., AP - Evan Vucci
Matangazo ya kibiashara

"Amerika haitatishwa," amesema rais wa Marekani. “Hatutazuiliwa na magaidi. Hatutawaacha wazuie operesheni yetu. Tutaendelea kna zoezi hilo", amsema rais wa Marekani. Joe Biden amebaini pia kwamba jeshi la Marekani litaondoka nchini afghanistan gosti 31 kama ilivyopangwa.

Joe Biden aapa "kuwasaka" washambuliaji wa Kabul

"Tutawatafuta popote walipo na tutawaangamiza," aamesema akiwaambia wahusika wa shambulio hilo, na kuongeza kuwa Marekani itajibu "kwa nguvu zote na usahihi". Askari hawa "ni mashujaa ambao walikuwa wakifanya kazi ya hatari na ya kujitolea kuokoa maisha ya watu wengine," amesema.

"Kufikia sasa, sijapewa uthibitisho kwamba kumekuwa na ushirikiano kati ya Taliban na kundila Islamic State", katika shambulio lililodaiwa na IS, pia amesema rais wa Marekani Joe Biden.

"Pia nimeagiza makamanda wangu kuandaa mipango ya kuteketeza mali ya IS-K, viongozi na vituo ya kundi hilo," Joe Biden amesema, akimaanisha tawi la IS nchini Afghanistan, kundi la Islamic State huko Khorasan.

 Kundi la Islamic State lilidai kuhusika na shambulio baya lililotokea Alhamisi wiki hii. IS inadai kwamba mmoja wa wapiganaji wake aliweza kukaribia kwenye "mita tano za jeshi la Marekani" kabla ya kulipua mkanda wake uliokuwa umejaa vilipuzi.

Wanajeshi kumi na tatu wa Marekani waliuawa na wengine 18 walijeruhiwa, kulingana na ripoti ya hivi karibuni kutoka Pentagon, makao makuu ya jeshi la Marekani.

Mlipuko mwingine ulitikisa mji mkuu wa Afghanistan karibu saa sita usiku, saa za nchini humo. Msemaji wa utawala wa Taliban Zabihullah Mujahid amesema mlipuko huo ulitokea wakati jeshi la Marekani lilikuwa likiteketeza vifaa vyake, madai ambayo jeshi la Marekani bado halijathibitisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.