Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-USALAMA

Afghanistan: Taliban wakubali Waafghan kuondoka nchini baada ya Agosti 31

Taliban wamekubali kwamba Waafghan wanaweza kuondoka nchini mwao baada ya tarehe ya mwisho ya kuondoka wanajeshi wa Marekani Agosti 31, amesema Jumatano wiki hii mwanadiplomasia wa Ujerumani ambaye anafanya mazungumzo na Taliban baada ya mkutano huko Qatar.

Waafghan katika kambi ya kijeshi ya Torrejon kama sehemu ya mchakato wa kuwaondoa raia wa Afghanistan nchini mwao kuwapeleka Madrid, Uhispania Jumanne, Agosti 24, 2021.
Waafghan katika kambi ya kijeshi ya Torrejon kama sehemu ya mchakato wa kuwaondoa raia wa Afghanistan nchini mwao kuwapeleka Madrid, Uhispania Jumanne, Agosti 24, 2021. © AP Photo / Andrea Comas
Matangazo ya kibiashara

Naibu mkuu wa kamati ya kisiasa ya Taliban huko Qatar Sher Abbas Stanekzai "amenihakikishia kuwa Waafghan wenye hati halali za kusafiri wataendelea kusafiri kwa ndege za kibiashara baada ya Agosti 31," Markus Potzel amesema kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Jumanne wiki hii rais wa Marekani Joe Biden alithibitisha kwamba tarehe ya mwisho ya wanajeshi wa Marekani kuondoka nchini Afghanistan ni Agosti 31, baada ya Taliban kupinga hoja yoyote ya kurefushwa kwa tarehe hiyo.

Hata hivyo rais wa Marekani alitoa kauli hiyo kwa sharti kuwa itaheshimu tarehe hiyo ya kuondoka nchini Afghanistan, ikiwa serikali mpya ya Afghanistan haitazuii raia wa Afghanistan ambao wanataka kuondoka nchini humo.

Lakini kwa kuheshimu tarehe hiyo ya mwisho "itategemea" ushirikiano wa Taliban "kuruhusu watu wanaotaka kusafiri kufika kwenye uwanja wa ndege", Joe Biden alitahadharisha, akiwaonya dhidi ya "kizuizi" chochote kwa operesheni hizi ngumu. Joe Biden alisema "ameomba Pentagon na Wizara ya Mambo ya Nje mipango ya dharura kurekebisha ratiba ikiwa italazimika".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.