Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-USALAMA

Taliban yalaani mashambulio katika eneo lililo chini ya "udhibiti" wa Marekani

Taliban "wamelaani vikali" mashambulio mabaya yaliyotokea Alhamisi hii Aosti 26 karibu na uwanja wa ndege wa Kabul, msemaji wao amesema, huku wakibaini kwamba mashambulizi hayo yamefanyika katika eneo lililo chini ya udhibiti wa jeshi la Marekani.

Moshi ukifumba katika mji wa Kabul baada ya milipuko yaliyotokea katika eneo karibu na uwanja wa ndege wa Kabul Alhamisi, Agosti 26.
Moshi ukifumba katika mji wa Kabul baada ya milipuko yaliyotokea katika eneo karibu na uwanja wa ndege wa Kabul Alhamisi, Agosti 26. AP - Wali Sabawoon
Matangazo ya kibiashara

"Falme ya Kiislam inalaani vikali mashambulio ya mabomu yanayowalenga raia katika uwanja wa ndege," Zabihullah Mujahid amesema kwenye ukurasa wake wa Twitter. Mlipuko huo ulitokea katika eneo ambalo wanajeshi wa Marekani wanahusika na usalama wa raia.

"Kulingana na Pentagon, milipuko miwili ilitokea karibu na uwanja wa ndege. Mashambulio hayo yamesababisha vifo vya watu wasiopungua sita, kulingana na shirika lisilo lakiserikali la Emergency kutoka Italia.

Mlipuko umetokea katika lango la kuingilia la abbey ambako vikosi vya Uingereza vimekuwa katika eneo hilo siku za karibuni.

Ni moja kati ya milango mitatu iliyokuwa imefungwa baada ya kuwepo tahadhari ya tishio la kigaidi.

Afisa wa Marekani ameliambia Shirika la habari la Reuters kuwa mlipuko huo ulisababishwa na mtu aliyejitoa muhanga.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.