Pata taarifa kuu
MEXICO-USHIRIKIANO

Mexico yapokea waandishi wa habari wa Afghanistan, waliofukuzwa na Marekani

Mexico imekuwa makao ya wakimbizi 130 wa Afghanistan ambao wamekimbia nchi yao katika siku chache zilizopita. Siku ya Jumatano, Mexico ilitangaza kuwasili kwa watu 124, waandishi wa habari ambao wamekuwa wanafanya kazi nchini Afghanistan kwa vyombo vya habari vya Marekani, wakiambatana na familia zao. Wakati Marekani ilikataa kuwapokea, serikali ya Mexico ilikubali kuwapokea.

Daraja la Ciudad Juarez ambalo ni mpaka kati ya Marekani na Mexico. Waandishi wa habari wa Afghanistan waliwasili kwa ndege.
Daraja la Ciudad Juarez ambalo ni mpaka kati ya Marekani na Mexico. Waandishi wa habari wa Afghanistan waliwasili kwa ndege. REUTERS - JOSE LUIS GONZALEZ
Matangazo ya kibiashara

Nchini Afghanistan, siku zinayoyoma kwa watu wanaotaka kuondoka nchini humo. Wanajeshi wa Marekani na wale kutoka nchi zingine za kideni wataondoka nchini Afghanistan Agosti 31.

Waafghan wengi naona maisha yao yako hatarini tangu Taliban kuchukua madaraka: wanawake, wanaharakati wa kisiasa na haki za binadamu, watu kutoka makabila madogo na waandishi wa habari hasa. RFI imekusanya ushuhuda wa mmoja wao:

“Tangu Taliban ichukue udhibiti wa mji wa Kabul, maisha yangu yamebadilika kabisa. Nilipoteza matumaini yangu, nilipoteza kazi yangu. Maisha ya kila siku pia yamenibadikia, masoko yako tupu, wanawake wanakaa ndani, hawatoki tena, benki zimefungwa, bei ya bidhaa imepanda. Watu wameishiwa pesa, hawawezi kununua chochote.

kama nitapata njia ya kuondoka hapa, nitaondoka 100% kwa sababu siwezi kufanya kazi chini ya mamlaka ya Taliban.

Siku mbili zilizopita, msemaji wao alisema, kama sijasahau , kwamba wangeunda mfumo wa vyombo vya habari kufanya kazi kulingana na sheria ya Kiislamu (Sharia). Tulikuwa huru, lakini sasa hatuwezi kufanya kazi tukiwa uhuru, tunachunguzwa. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.