Pata taarifa kuu
KENYA-UCHAGUZI

Upinzani wakataa matokeo ya uchaguzi Kenya

Muungano wa mgombea wa upinzani katika uchaguzi wa urais nchini Kenya, Raila Odinga ulitangaza usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano kwamba unafutilia mbali matokeo yamuda yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi.

Raila Odinga wakati wa mkutano na vyombo vya habari usiku wa tarehe 8 kuamkia 9 Agosti 2017.
Raila Odinga wakati wa mkutano na vyombo vya habari usiku wa tarehe 8 kuamkia 9 Agosti 2017. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na matokeo hayo rais anaye maliza muda wake Uhuru Kenyatta, amepata kura nyingi dhidi ya mshindani wake mkubwa.

Raila Odinga mwenyewe aliviambia vyombo vya habari kwamba hakubaliani na "matokeo ya uwongo": "Matokeo haya ni ya uwongo, ni kweli. Kile kinachotokea ni aibu, na hayo yanafanywa katika kutokuzingatia sheria.

Bw Odinga asema kabla ya matokeo yoyote kutangazwa, IEBC inafaa kuwapa maajenti wa vyama Fomu 34A kutoka vituoni.

"Mfumo umeacha kufanya kazi. Sasa ni mitambo inayopiga kura. IEBC wamesema kwamba hakuna chama chochote kilichopinga matokeo. Lakini vyama vitapingaje matokeo bila kujua asili yake? Ni fomu 34A pekee zinazoonesha chanzo cha matokeo," Bw Odinga amesema.

Wakala mkuu wa muungano huo wa upinzani, naibu waziri mkuu wa zamani Musalia Mudavadi alikuwa awali amehutubia wanahabari na kutaja matokeo yanayotangazwa na tume hiyo kama utapeli.

"Kwa sasa tunaingia katika awamu muhimu zaidi ya mzunguko wa uchaguzi," alionya mkuu wa Tume ya Uchaguzi (IEBC), Wafula Chebukati, mapema jioni, na kuwataka Wakenya kuwa na subira. Tume ya uchaguzi ilitetea chaguo lake la kuendelea kutangaza matokeo ya mwanzo ya uchaguzi kwa ajili ya "uwazi kwa wapiga kura na Wakenya."

Uchunguzi wa awali, ulionyesha kuwa wagombea wote wawili walikua wakikaribiana kwa kura katika siku ya mwisho ya kampeni.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.