Kenyatta na Odinga wapiga kura
Wapiga kura zaidi ya milioni 19 nchini Kenya walipiga kura siku ya Jumanne kumchagua rais wao. Rais Uhuru Kenyatta na mpinzani wake mkuu Raila Odinga walipiga kura asubuhi.
Imechapishwa:
Cheza - 01:46
Raila Odinga alipiga kura kwenye kituo cha Olimpiki kilichoko Kibera Kusini Magharibi mwa Nairobi.Uhuru Kenyatta alipiga kura katika kituo cha Mutomo, Kaskazini Magharibi mwa Nairobi.
Kenyatta amekariri kuwa akishindwa uchaguzi atakubali matokeo.
Haya hapa ni mahojiano kati ya mwandishi wa RFI-Kiswahili James Shimanyula na rais anayemaliza muda wake Uhuru Kenyatta:
James: Rais habari ya asubuhi.
Uhuru Kenyatta: Salama habari yako
James: Kila la heri.
Uhuru Kenyatta: Asante sana twashukuru.
James: Unafikiria kwamba bado msimamo ni kwamba utapasua?
Uhuru Kenyatta: Msimamo ni huo huo tu.
James: Na umekubali kuwa utakubali matokeo?
Uhuru Kenyatta: Mimi nitakubali matokeo.
James: Rais Kenyatta tayari amewekewa kidole. Kuna wakati ambapo wasiwasi unakuzunguka kwa kichwa?
Uhuru Kenyatta: Ngoja nimalize na hawa tafadhali.
James: Tuko na wewe asante.