Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA-UCHAGUZI

Rais Kenyatta na Odinga wasema watakubali matokeo ya Uchaguzi Mkuu

Rais Uhuru Kenyatta na mpinzani wake Mkuu Raila Odinga walipiga kura mapema hivi leo.

Rais Uhuru Kenyatta and Raila Odinga wakipiga kura Agosti 8 2017
Rais Uhuru Kenyatta and Raila Odinga wakipiga kura Agosti 8 2017 Daily Nation
Matangazo ya kibiashara

Mwandishi wetu James Shimanyula alishuhudia rais Uhuru Kenyatta akipiga kura katika jimbo la Gatundu Kusini.

Mgombea wa NASA Raila Odinga naye alipiga kura katika jimbo la Kibra jijini Nairobi.

Wagombea hawa wawili wamesema wana imani kubwa ya kushinda lakini wakipoteza watakubali matokeo.

Soma mahojiano kati ya Mwandishi wa RFI Kiswahili James Shimanyula na rais Uhuru Kenyatta:-

Mwandishi wetu JAMES SHIMANYULA: Rais habari ya asubuhi, Rais habari ya asubuhi, habari ya asubuhi Rais.

UHURU KENYATTA: Salama habari yako

JAMES: Kila la heri.

UHURU KENYATTA: Asante sana twashukuru.

JAMES: Unafikiria kwamba bado msimamo ni kwamba utapasua?

UHURU KENYATTA: Msimamo ni huo huo tu.

JAMES: Na umekubali kuwa utakubali matokeo?

UHURU KENYATTA: Mimi nitakubali matokeo.

JAMES: Rais Kenyatta tayari amewekewa kidole. Kuna wakati ambapo wasiwasi unakuzunguka kwa kichwa?

UHURU KENYATTA: Ngoja nimalize na hawa tafadhali.

JAMES: Tuko na wewe asante.

Nilimhoji pia Margaret, mkewe Rais Kenyatta

JAMES: Mama habari ya asubuhi? How are you?

JAMES: Ukoje, hali yako.

MARGARET KENYATTA: I’m very well thanks. Sorry?

Anasema ana furaha. Samahani, ananiambia.

JAMES: Are you confident that victory is just dangling?

Je una hakika mtashinda na ushindi upo macho penu?

MARGARET KENYATTA: I believe so.

Ninaamini hivyo, alisema Mkewe Rais Kenyatta.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.