Pata taarifa kuu
KENYA

Tume ya Uchaguzi nchini Kenya yalaani mpango wa upinzani kuwa na kituo cha kujumuisha matokeo

Tume ya Uchaguzi nchini Kenya imesema ndio iliyo na mamlaka ya kujumuisha na kutangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu nchini humo.

Maofisa wa tume huru ya uchaguzi nchini Kenya, IEBC, wakiwa katika shughuli ya kuandikisha wapiga kura wapya, 16 Januari 2017.
Maofisa wa tume huru ya uchaguzi nchini Kenya, IEBC, wakiwa katika shughuli ya kuandikisha wapiga kura wapya, 16 Januari 2017. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Kauli hii imetolewa na Mwenyekiti wa Tume hiyo Wafula Chebukati baada ya muungano wa upinzani NASA kutangaza mwishoni mwa wiki kutangaza kuwa itakuwa na kituo chake cha kujumuisha matokeo.

Chebukati amewataka wanasiasa wa upinzani kuiamini Tume hiyo na kuwahikikishia kuwa mawakala wao watapata fursa ya kuthathmini matokeo yote yatakayotolewa baada ya zoezi la kupiga kura tarehe 8 mwezi Agosti mwaka huu.

Kigogo wa upinzani Raila Odinga amesema, upinzani umeweka mikakati ya kuwa na kituo chake cha kujumuisha matokeo na kuyatangaza na kusisitiza kuwa hakuna atakayewazuia kufanya hivyo.

Odinga amesema kuwa kila kituo cha kupigia kura kutakuwa na mawakala wao watano watakaohakikisha kuwa kura za upinzani zimelindwa.

Muungano wa NASA hivi karibuni umekuwa ukihoji utayari wa Tume ya Uchaguzi nchini humo na hata kusema hauwaamini Makamishena hao.

Hata hivyo, Tume ya Uchaguzi inasema zoezi hilo litakuwa huru na haki na ipo tayari kuandaa Uchaguzi huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.