Pata taarifa kuu
BURUNDI-NJAA-USALAMA

Ripoti ya kibinadamu yatahadhari uhaba wa chakula nchini Burundi

Ripoti ya pamoja ya washirika katika suala la kibinadamu, serikali ya Burundi na wafadhili yenye jina la "Taswira ya mahitaji ya kibinadamu mwaka 2017" imetahadhari kuhusu ukosefu wa chakula unaowakabili raia wa taifa hilo dogo linalokumbwa na mgogoro wa kisiasa.

Katika mgahawa wa pamoja wa Rema katika hospitali ya moani Ruyigi, Mei 2012.
Katika mgahawa wa pamoja wa Rema katika hospitali ya moani Ruyigi, Mei 2012. Photo : RFI / Matthieu Millecamps
Matangazo ya kibiashara

Ripoti hiyo iliyotolewa mwezi Januari inatoa wito kwa jumuiya ya kimataiofa kuipa Burundi Dola milioni 73, ili kukabiliana na hali ya kibinadamu inayoendelea "kuzorota kwa kasi", wakati ambapo robo ya wananchi wa taifa hilo wanahitaji msaada wa kibinadamu. Na ripoti hii imetumia neno "kutisha" kuelezea hali hiyo.

Serikali ya Burundi imeshindwa kutumia neno "njaa" na kuamua kutumia neno "ukosefu wa chakula". Hata hivyo serikali ya Burundi imebaini kwamba hali imeanza kuwa shwari baada ya kuonekana mavuno mazuri msimu huu na mshikamano wa kitaifa. Neno "njaa" limepigwa kwenye ripoti hii, lakini taarifa mbalimbali kutoka Burundi zaeleza kwamba baadhi ya raia kutoka mikoa mbalimbali wameyakimbia makaazi yao na wengine kuuza nyumba zao kutokana na njaa ambayo imesababishwa na ukame.

Milioni tatu ya watu wanaoishi Burundi walihitaji misaada ya kibinadamu mwishoni mwa mwaka 2016, ikiwa ni mara tatu zaidi ya mwaka mmoja uliopita, imesema ripoti hiyo ambayo imetoa tahadhari kwa haraka kwa kuzorota kwa hali hiyo. Kati yao, zaidi ya watu 800,000 walikuwa katika "ukosefu mkubwa wa chakula," neno lililopasishwa kisiasa ambalo linaficha dhiki kubwa ya watu ambao wanahitaji msaada wa haraka.

Mgogoro usiokua na mwisho

Sababu ya kuzorota kwa hali hiyo ni mabadiliko ya hali ya hewa, lakini pia kuzorota kwa hali ya kijamii na kiuchumi kama matokeo ya mgogoro mkubwa unaoikabili nchi hii kwa karibu miaka 2, imesema ripoti hiyo, ambayo ni matunda ya kazi ya pamoja kati ya wadau katika suala la kibinadamu nchiniBurundi, serikali na wafadhili.

Lakini mgogoro huu si wa chakula pekee. Hali imeendelea kuzorota katika ngazi zote, Ulinzi, Elimu, Upatikanaji wa maji safi, au Afya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.