Pata taarifa kuu
BURUNDI-SIASA

Wanasiasa wa Burundi waendelea kushauriana kuhusu maswala tata

Mazungumzo ya amani ya Burundi kujaribu kuleta pande pinzani katika meza ya mazungumzo ya moja kwa moja, yanaendelea mjini Arusha nchini Tanzania.

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza RFI Hausa
Matangazo ya kibiashara

Mratibu wa mazungumzo hayo, ambaye ni rais wa zamani wa Tanzania Benjamin Mkapa, alikuwa amepanga kuwa mazungumzo hayo yamalizike siku ya Jumamosi lakini kwa sababu ya mashauriano yanayoendelea, yatamalizika siku ya Jumapili.

Mwandishi wa RFI Ali Bilal ambaye yuko mjini Arusha anasema, wajumbe kutoka pande mbili bado wanazungumza kukubaliana kuhusu maswala muhimu watakayojadili katika mazungumzo ya ana kwa ana.

Maswala tata ambayo yanaonekana kukubaliwa na pande zote mbili ni pamoja na hatima ya wakimbizi ambao waliondoka nchini Burundi kwa sababu za kisiasa.

Maswala mengine tata ambayo yanaonekana kukubaliwa na pande zote ni kuhusu kupata mwafaka wa hali ya kisiasa nchini humo na namna ya kukabiliana na vikwazo vya kiuchumi, vilivyowekwa na hasa Umoja wa  Ulaya.

Hata hivyo, muda wa wajumbe hawa kuendelea kushauriana unatiliwa shaka kwa sababu kile kinachoonekana kuwa unachelewesha kuanza kwa mazungumzo ya ana kwa ana.

Baada ya maswala yote tata kukubaliwa, msuluhishi wa mazungumzo haya ambaye ni rais wa Uganda Yoweri Museveni atachukua jukumu ya kuongoza mazungumzo ya ana kwa ana.

Jumuiya ya Afrika Mashariki imeshutumiwa kwa kuchukua muda mrefu kutatua mzozo huu wa Burundi, huku lawama zingine zikiwaendea wanasiasa wa Burundi kwa kutoonesha utayari wa kupatikana kwa mwafaka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.