Pata taarifa kuu
BURUNDI-ARUSHA

Warundi waandamana kupinga mazungumzo ya Arusha

Melfu ya warundi walijikusanya katika viunga vya jiji la bujumbura jana jumamosi kuandamana kupinga mazungumzo ya amani yaliyolenga kumaliza mzozo unaolikabili taifa hilo,mazungumzo ambayo upande wa serikali haukushiriki.

Maandamano mjini Bujumbura cnhini Burundi
Maandamano mjini Bujumbura cnhini Burundi STRINGER / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo ya Arusha nchini Tanzania yameendelea zikiwa ni juhudi za kumaliza mzozo uliozuka baada ya raisi piere nkurunziza kuamua kuwania muhula wa tatu mnamo April 2015.

Hata hivyo serikali iligom akukaa meza moja na muungano wa upinzani chini ya mwamvuli wa CNARED na kwenda mbali zaidi kuomba watiwe nguvuni na mamlaka nchini Tanzania.

Mmoja kati ya waandaaji wa maandamano hayo ya amnai Gilbert Becaud Njangwa aliiambia AFP kuwa wamefanya maandamano hayo kuitaka serikali ya burundi kutounga mkono matoeo ya mazungumzo ya Arusha ambayo yamehudhuriwa na maafui wa demokrasia ya Burundi.

Mazungumzo ya kusaka amani nchini Burundi hii leo yanaingia katika siku yake ya nne na ya mwisho ambapo makundi mbalimbali ya wanasiasa katika mazungumzo hayo yatawasilisha tathimini ya maswala nane waliopewa na msuluhisi ambayo walitakiwa kuyakusanya katika hoja nne.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.