Pata taarifa kuu
BURUNDI-MAZUNGUMZO-SIASA

Mazungumzo ya amani yafanyika licha ya serikali ya Burundi kukataa kushiriki

Wanasiasa wa Burundi wanakutana mjini Arusha chini Tanzania chini ya mratibu wa mazungumzo hayo ya amani, rais wa Zamani wa Tanzania Benjamin William Mkapa kujaribu kutafuta suluhu ya mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini humo.

Mazungumzo baina ya Burundi yalizinduliwa rasmi nchini Uganda Jumatatu, Desemba 28, kupitia upatanishi wa rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni.
Mazungumzo baina ya Burundi yalizinduliwa rasmi nchini Uganda Jumatatu, Desemba 28, kupitia upatanishi wa rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni. RFI-KISWAHILI
Matangazo ya kibiashara

Mgogoro huo umesababisha maelfu ya raia wa Burundi kulitoroka taifa lao na wengine wanaokadiriwa kufikia elfu moja kupoteza maisha.

Wakati mazungumzo ya amani ya burundi yakianza jijini arusha Tanzania makundi mbalimbali ya kijamii toka nchini humo yametaka kuwepo kwa ushirikishwaji mpana hasa kwa wanawake na makabila mengine madogo nchini humo, ikiwa ni pamoja na kundi la watu kutoka jamii ya Waswahili.

Serikali ya Burundi imesema haitashiriki katika mazungumzo ya amani yanayoanza Alhamisi wiki hii kati yake na wanasiasa wa upinzani, mjini Arusha nchini Tanzania.

Hata hivyo muungano wa wanasiasa wa upinzani CNARED umekubali kushiriki katika mazungumzo hayo.

Msemaji wa serikali Philippe Nzobonariba amesema Bujumbura haijaridhiswa na namna mazungumzo haya yalivyoandaliwa lakini pia uwepo wa mshauri wa Umoja wa Mataifa Benomar Jamal.

Hatua hii ya serikali ya Burundi, inarudisha nyuma upatikanaji wa suluhu kuhusu mzozo wa kisiasa nchini humo hasa wakati huu ambao muungano wa vyama vya upinzani CNARED ambao viongozi wake wanaoishi nchi wakikubali kuhudhuria mazungumzo hayo, yanayoongozwa na Mratibu ambaye ni rais wa zamani wa Tanzania Benjamin Mkapa.

Rais mstaafu wa Tanzania anataka kujadiliwa kwa mara ya kwanza "masuala nyeti", kama vile muhula wa tatu wa Rais Pierre Nkurunziza unaoendelea kuzua utata na "uundwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa," amesema mwanadiplomasia wa Afrika ambaye hakutaka jina lake litajwe.

Majaribio ya kuwaleta kwenye meza moja ya mazungumzo serikali ya Burundi na upinzani walio uhamishoni hadi sasa yameshindwa. Serikali ya Bujumbura imekataa mpaka sasa kuketi kwenye meza ya mazungumzo na Cnared licha ya shinikizo na vikwazo kutoka jumuiya ya kimataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.