Pata taarifa kuu

Tanzania yathibitisha kifo cha raia wake aliyeuawa na kundi la Hamas nchini Israel

Wizara ya Mambo ya nje nchini Tanzania, imethibitisha kifo cha mmoja wa raia wake, aliyeuawa baada ya kutekwa na kundi la Hamas, lililovamia Kusini mwa Israeli, Oktoba tarehe 

Makutano ya barabara ya mwalimu Nyerere mjini Dodoma, mji mkuu wa kisiasa wa Tanzania.
Makutano ya barabara ya mwalimu Nyerere mjini Dodoma, mji mkuu wa kisiasa wa Tanzania. DR
Matangazo ya kibiashara

 

Waziri wa Mambo ya nje, January Makamba kupitia ukurasa wake wa kijamii wa X, amethibitisha kifo cha raia huyo wa Tanzania, aliyetajwa kuwa Joshua Mollel, aliyekuwa anasoma nchini Israeli. 

Makamba ameeleza kuwa, serikali ya Israeli imeiambia Tanzania kuwa, Mollel mwenye umri wa miaka 21 ambaye alipoteza mawasiliano na ndugu zake, aliuawa mara tu baada ya kutekwa na kundi la Hamas. 

Serikali ya Tanzania imesema imewasiliana na família ya Mollel, na inatarajiwa kutuma ujumbe nchini Israeli ili kupata taarifa zaidi kuhusu mpendwa wao. 

Baada ya tukio hilo, Israeli iliwataja raia wawili wa Tanzania, waliokuwa wametekwa na Hamas, akiwemo Joshua Mollel.  

Mtanzania mwingine, Clemence Felix Mtenga mwenye umri wa miaka 22, ambaye pia alitangazwa kuuawa mwezi uliopita. 

Wawili hao waliouawa baada ya kutekwa, walikuwa miongoni mwa Watanzania 260 waliokwenda Israel kupata mafunzo kuhusu kilimo cha kisasa. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.