Pata taarifa kuu

Eli Cohen: Israel itaendeleza vita vyake dhidi ya Hamas 'kwa msaada wa kimataifa au la'

Israel inakabiliwa na shinikizo kutoka kwa washirika wake wa karibu, hasa Marekani, ambayo imeshutumu kupitia Rais wake Joe Biden "mashambulio ya kiholela" na kukataa kwa Israeli "suluhisho la serikali mbili". Hata hivyo, mapigano yanaendelea kupamba moto na jeshi la Israel lilirekodi siku yake mbaya zaidi siku ya Jumanne huku wanajeshi 10 wakiuawa katika safu zake.

Moshi ukipanda angani juu ya Jenin, Ukingo wa Magharibi, wakati wa operesheni ya jeshi la Israeli, Jumatano, Desemba 13, 2023.
Moshi ukipanda angani juu ya Jenin, Ukingo wa Magharibi, wakati wa operesheni ya jeshi la Israeli, Jumatano, Desemba 13, 2023. AP - Majdi Mohammed
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel, Eli Cohen, amehakikisha siku ya Jumatano kwamba licha ya wito wa jumuiya ya kimataifa wa kusitisha mapigano huko Gaza, taifa hilo la Kiyahudi halina nia ya kukatiza operesheni yake: "Israel itaendeleza vita dhidi ya Hamas, kwa msaada wa kimataifa au la. Kusitishwa kwa mapigano katika hatua hii itakuwa zawadi kwa shirika la kigaidi la Hamas na kuliruhusu kuibuka tena na kutishia raia wa Israeli. "

Wakati huo huo Mshauri wa usalama wa kitaifa kutoka ikulu ya White House Jake Sullivan atazuru Israel siku ya Alhamisi na Ijumaa, afisa mkuu wa Marekani amesema, baada ya tofauti kati ya washirika hao wawili kudhihirika.

Atakutana na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, "baraza la kivita" la Israel pamoja na Rais Isaac Herzog, kulingana na taarifa kutoka kwa Adrienne Watson, msemaji wa Baraza la Usalama la Taifa, chombo kinachohusishwa moja kwa moja na Rais wa Marekani Joe Biden.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.