Pata taarifa kuu

Marekani yatiwa wasiwasi baada ya makala kuhusu matumizi ya Israel ya fosforasi nyeupe

Serikali ya Marekani imesema ina "wasiwasi" baada ya kuchapishwa kwa makala katika Gazeti la Washington Post, ambalo linadai, kulingana na uchanganuzi wa vipande kama uhahidi, kwamba Israel ilitumia mabomu ya fosforasi nyeupe yaliyotengenezwa nchini Marekani wakati wa mashambulizi kusini mwa Lebanon mwezi Oktoba. "Tutauliza maswali ili kujaribu kujua zaidi kidogo,” amesema John Kirby, msemaji wa Baraza la Usalama la Kitaifa la Ikulu ya White House.

Makombora ambayo yanaonekana kuwa ya fosforasi nyeupe kutoka jeshi la Israel yanalipuka huko Dahaira, kijiji nchini Lebanon kinachopakana na Israel, Oktoba 16, 2023.
Makombora ambayo yanaonekana kuwa ya fosforasi nyeupe kutoka jeshi la Israel yanalipuka huko Dahaira, kijiji nchini Lebanon kinachopakana na Israel, Oktoba 16, 2023. AP - Hussein Malla
Matangazo ya kibiashara

Mabomu ya fosforasi ni silaha za moto ambazo matumizi yake yamepigwa marufuku dhidi ya raia, lakini sio dhidi ya malengo ya kijeshi, kulingana na Mkataba uliotiwa saini mnamo mwaka 1980 huko Geneva. Matumizi "halali" ya fosforasi nyeupe yanalenga "kuangaza na kutoa moshi ili kusitisha shughuli," John Kirby amesema. "Tunaposambaza vifaa kama vile fosforasi nyeupe kwa jeshi lingine, ni kwa ajili yake kutumika kwa njia hii halali na kwa mujibu wa sheria ya migogoro ya silaha," ameongeza.

"Fosforasi nyeupe inaweza kutumika kihalali katika ngazi ya kijeshi lakini si dhidi ya raia," pia amekumbusha msemaji wa wizara ya usalama ya Marekani, Matthew Miller, akihakikishia kwamba utawala wa Biden ulikuwa unatafuta kupata " taarifa ya ziada ". Marekani ndiyo msambazaji mkuu wa zana za kijeshi kwa Israel na Rais wa Marekani Joe Biden aliahidi kuunga mkono kikamilifu mashambulizi ya Israel dhidi ya Hamas.

Lebanon imeishutumu Israel kwa wiki kadhaa kwa kutumia fosforasi nyeupe wakati wa mashambulizi dhidi ya Hezbollah kusini mwa nchi hiyo, ambayo yalisababisha moto mkubwa. Shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Amnesty International, kwa upande wake, limedai kuwa na "ushahidi wa matumizi haramu ya Israel ya fosforasi nyeupe" kati ya Oktoba 10 na 16, na kutaka "uchunguzi wa uhalifu wa kivita". Katikati ya mwez Oktoba, Human Rights Watch pia iliishutumu Israel kwa kutumia fosforasi nyeupe huko Gaza na Lebanon. "Tunakanusha madai haya," msemaji wa jeshi la Israel alijibu mara moja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.