Pata taarifa kuu

Urusi yatoa wito kwa Waisraeli na Wapalestina kuacha kusitisha uhasama

Moscow imewataka Waisraeli na Wapalestina kuzuia "kuongezeka" kwa ghasia na kutafuta maelewano, baada ya mashambulizi ya Israel dhidi ya Lebanon na Ukanda wa Gaza kujibu mashambulizi ya roketi dhidi ya ardhi yake. 

Picha hii iliyopigwa kutoka mji wa Siraeli wa Ashkelon inaonyesha roketi zilizorushwa kutoka Ukanda wa Gaza mnamo Agosti 7, 2022.
Picha hii iliyopigwa kutoka mji wa Siraeli wa Ashkelon inaonyesha roketi zilizorushwa kutoka Ukanda wa Gaza mnamo Agosti 7, 2022. AFP - JACK GUEZ
Matangazo ya kibiashara

Hayo yanajiri wakati wanawake wawili wa Kiisraeli waliuawa na mama yao kujeruhiwa vibaya mapema siku ya  Ijumaa katika shambulio katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa, baada ya mashambulio ya Israeli dhidi ya Ukanda wa Gaza na kusini mwa Lebanon, tukio la hivi karibuni katika kuongezeka kwa mvutano katika Mashariki ya Kati.

Urusi yatoa wito kwa Waisraeli na Wapalestina kuacha kusitisha uhasama

Moscow imewataka Waisraeli na Wapalestina kuzuia "kuongezeka" kwa ghasia na kutafuta maelewano, baada ya mashambulizi ya Israel dhidi ya Lebanon na Ukanda wa Gaza kujibu mashambulizi ya roketi dhidi ya ardhi yake. 

"Tunatoa wito kwa pande zinazohusika kujiepusha na makabiliano yoyote na kuchukua hatua ili kuzuia kuongezeka kwa uhasama, kumaliza ghasia na kufikia usitishaji wa kudumu wa mapigano," Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi imesema katika taarifa.

Israel ilisema ililenga ngome za vuguvugu la Palestina Hamas huko Gaza na Lebanon, kujibu shambulizi la makumi ya roketi dhidi ya ardhi yake.

Baada ya utulivu katika mzozo wa Israel na Palestina ulioshuhudiwa tangu kuanza kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kuanza mnamo Machi 23, mapigano ya Jumatano kati ya vikosi vya Israeli na Palestina katika msikiti wa Al-Aqsa huko Jerusalem, eneo la tatu takatifu katika Uislamu, yalichochea uhasama mkubwa.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema majeshi ya Israel "yalilazimishwa kuchukua hatua ili kurejesha utulivu" dhidi ya "wanamgambo wenye msimamo mkali".

Siku ya Ijumaa, wanawake wawili wenye umri wa miaka ishirini waliuawa na wa tatu "kujeruhiwa vibaya" katika shambulio katika Ukingo wa Magharibi, shirika la Magen David Aadom, sawa na shirika la Msalaa Mwekundu nchini Israel.

Jeshi la Israel limesema waliouawa ni Waisraeli na kwamba gari lao lilipigwa risasi kwenye makutano ya Hamra kaskazini mashariki mwa Ukingo wa Magharibi, eneo linalokaliwa na Israel tangu 1967.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.