Pata taarifa kuu

Watu wawili wameuawa baada ya kushambuliwa katika Ukingo wa Magharibi

NAIROBI – Raia wawili wa Israeli ambao ni dada, wameuawa, na mama yao kujeruhiwa katika ukingo wa Magharibi, saa chache baada ya jeshi la nchi hiyo kushambulia Gaza na Lebabon, kufuatia hatua ya kundi la Kipalestina la Hamas kurusha roketi katika ardhi yake. 

Wito umetolewa wa kusitishwa kwa makabiliano kati ya pande hasimu katika Ukingo wa Magahribi
Wito umetolewa wa kusitishwa kwa makabiliano kati ya pande hasimu katika Ukingo wa Magahribi AFP - AHMAD GHARABLI
Matangazo ya kibiashara

Mauaji hayo yamesabishwa na watu waliokuwa wamejihami kwa silaha kufyatulia risasi, gari lililokuwa linawasafirisha raia hao wa Israeli, kitendo ambacho kimeongeza hali ya wasiwasi. 

Alfajiri ya kuamkia leo, jeshi la Israeli lilitekeleza mashambulio ya angaa katika eneo la Gaza na Kusini mwa Lebanon, kulenga ngome za kundi la Hamas. 

Israeli imesema ilichukua hatua hiyo, kujibu hatua ya kundi hilo kurusha maroketu 34 yaliyotokea Lebanon, kuelekea katika eneo la Kaskazini mwa nchi yake. 

Hili limekuwa shambulio baya zaidi katika ardhi ya Israeli kutoka Lebanon, wakati kundi la Hezbollah, liliporusha maroketi mwaka 2006 na hii ndio mara ya kwanza kwa jeshi la Israeli kushambulia ardhi ya Lebanon tangu Aprili 2022. 

Hali  ya wasiwasi ilianza kushuhudiwa  baada ya Polisi wa Israeli kukabiliana na Wapaletuna ndani ya Msikiti wa Al-Aqsa, huku Jumuiya ya Kimataifa, ikiomba utulivu. 

Waziri Mkuu Benjemin Netanyahu, amesema jeshi la Israeli itaendelea kulipiza kisasi na kundi la Hamas litarajie gharama kubwa. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.