Pata taarifa kuu

Jeshi la Israel laishambulia Gaza

NAIROBI – Jeshi la Israel usiku wa kuamkia leo limetekeleza mashambulio mfululizo kwenye ukanda wa Gaza na Lebanon, likisema linalenga ngome za wapiganaji wa Hamas baada ya roketi kadhaa kurushwa kwenye ardhi yake.

Israeli imeishambulia gaza kwa makombora
Israeli imeishambulia gaza kwa makombora AFP - MOHAMMED ABED
Matangazo ya kibiashara

Mashambulio ya Israel yalianza saa kumi na nusu kwa saa za nchi hiyo, ambapo yalilenga eneo la ukingo wa Gaza na kusini mwa nchi ya Lebanon, imesema taarifa ya jeshi la Israel.

Kwa mujibu wa mashuhuda milipuko ilisikika kuanzia usiku, saa chache baada ya wapiganaji wanaodhaniwa kuwa ni wa Hamas kurusha makombora kadhaa kwenye ardhi ya Israel.

Israel inasema zaidi ya roketi 30 zilirushwa kutokea eneo la Lebanon.

Mzozo kati ya Israel na Palestina umeshika kasi tangu kuanza kwa Kwaresma na mfungo wa mwezi wa Ramadhani, hatua ambayo imekashifiwa vikali na Jumuiya ya kimataifa.

Hatua hii ya Israel ikija  muda mfupi baada ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kutoa taarifa ya video akiahidi kwamba maadui wa nchi yake "watalipa gharama kubwa kutokana na uchokozi wowote".

Wito umendelea kutolewa na jamii ya kimataifa kwa pande zinazohasimiana katika mzozo huo kumaliza makabiliano na kutafuta suluhu la mzozo huo mwa muda mrefu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.