Pata taarifa kuu

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa litaamua juu ya usitishaji vita Gaza siku ya Jumanne

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa pengine litapiga kura siku ya Jumanne kuhusu rasimu ya azimio linalotaka kusitishwa mara moja kwa mapigano huko Gaza ambako wapiganaji wa Hamas na wanajeshi wa Israel wanapambana, shirika la habari la REUTERS limeripoti likinukuu chanzo cha kidiplomasia.

Wanajeshi wa Israel wakitayarisha silaha na magari kabla ya kuingia Ukanda wa Gaza, Desemba 10, 2023.
Wanajeshi wa Israel wakitayarisha silaha na magari kabla ya kuingia Ukanda wa Gaza, Desemba 10, 2023. AFP - GIL COHEN-MAGEN
Matangazo ya kibiashara

Kura hii itakuja baada ya Marekani kupinga kwa kutumia kura yake ya turuhu azimio kuhusu kusitishwa kwa mapigano huko Gaza siku ya Ijumaa.

WHO yapitisha azimio la kutaka msaada wa haraka wa kibinadamu kwa Gaza

Bodi ya Utendaji ya Shirika la Afya Duniani (WHO) imepitisha kwa makubaliano azimio la kutaka msaada wa haraka wa kibinadamu kwa Gaza. Wakati Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilishindwa kupitisha azimio kuhusu kusitishwa kwa mapigano kati ya Israel na Hamas, kutokana na kura ya turufu ya Marekani, nchi 34 wanachama wa Baraza la Utendaji la WHO zote zinataka "kupitishwa kwa haraka, endelevu na bila vikwazo misaada ya kibinadamu" katika Umoja wa Mataifa kwa Ukanda wa Gaza.

Hamas inasema hakuna mateka atakayeondoka Gaza "hai" bila "mazungumzo"

Hamas imeonya siku ya Jumapili kwamba hakuna mateka hata mmoja waliotekwa nyara wakati wa shambulio la Oktoba 7 na ambao bado wanashikiliwa katika Ukanda wa Gaza atakayeondoka "hai" bila mazungumzo na bila "kukidhi matakwa" yakundi hilo la wanamgambo la Palestina. "Wala adui wa kifashisti na uongozi wake wa kiburi, au wafuasi wake, wataweza kuwaokoa wafungwa wao wakiwa hai bila kufanya mazungumzo, na bila kukidhi matakwa ya Hamas," Abou Obeida, msemaji wa tawi la kijeshi la Hamas amesema katika video.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.