Pata taarifa kuu

Mapigano makali yarindima Gaza katikati ya mazungumzo kuhusua kuachiliwa kwa mateka

Wakati mapigano makali yakitokea katikati mwa Jiji la Gaza siku ya Jumapili, mazungumzo yanaendelea kuwaachilia mateka. Vikosi vya Israel bado "vinapanua" operesheni zao dhidi ya Hamas kaskazini mwa Ukanda wa Gaza siku ya Jumatatu katikati ya mazungumzo yenye lengo la kuwaachilia mateka walioko mikononi mwa kundi la  kwa kubadilishana na kusitishwa mapigano.

Watoto wa Kipalestina waliokimbilia katika hospitali ya Nasser katika kambi ya wakimbizi ya Khan Younes kusini mwa Gaza, Oktoba 29, 2023.
Watoto wa Kipalestina waliokimbilia katika hospitali ya Nasser katika kambi ya wakimbizi ya Khan Younes kusini mwa Gaza, Oktoba 29, 2023. REUTERS - MOHAMMED SALEM
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na Wizara ya Afya ya Hamas, watu 41 wa familia moja waliuawa katika shambulio la anga la Israeli dhidi ya nyumba yao huko Jabaliya. Shirika la Wafa la Palestina liliripoti shambulio la anga wakati wa usiku kwenye hospitali ya Indonesia, kaskazini mwa mji wa Gaza. Jeshi la Israel limedai kuendelea "kupanua operesheni zake katika maeneo mapya ya Ukanda wa Gaza", hasa katika eneo la Jabaliya. Wanajeshi watano wa Israel waliuawa, na kufanya idadi ya wanajeshi waliouawa Gaza kufikia 64 tangu kuanza kwa vita, jeshi la Israel limesema.

Watoto 31 waliozaliwa kabla ya wakati wao wahamishwa

Katika siku za hivi karibuni, hali ya wasiwasi imetanda katika hospitali ya Al-Shifa, kubwa zaidi katika Ukanda wa Gaza, ambayo sasa iko chini ya udhibiti wa jeshi la Israel, ambalo lilisema kuwa limegundua handaki lenye urefu wa mita 55 na kuchimba kina cha mita 10 likiwa na "bunduki za kurusha guruneti. , vilipuzi na bunduki aina ya Kalashnikov”. Jeshi la Israel lilitoa picha za Jumapili jioni zilizowasilishwa kama zikitoka kwenye kamera za uchunguzi za hospitali ya Al-Shifa huko Gaza.

Zaidi ya watoto 30 wanaozaliwa kabla ya wakati wao

walihamishwa siku ya Jumapili kutoka hospitali ya Al-Shifa hadi Rafah (kusini mwa Gaza), ili kupata "huduma ya haraka katika chumba cha wagonjwa mahututi", amesema mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Tedros Adhanom Ghebreyesus. "Watoto hawa waliteseka sana" na walipata "athari kubwa," mkurugenzi mkuu wa hospitali katika Ukanda wa Gaza, Mohammed Zaqout, ameelezea kwa vyombo vya habari, akionyesha kuwa watoto wanane walikufa kwa kukosa matunzo kabla ya uhamisho wao, ikiwa ni pamoja na. wawili siku ya Jumapili asubuhi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.