Pata taarifa kuu

Israel na Hamas wafikia makubaliano ya kusitisha mapigano ili kuachiliwa huru mateka

Baada ya wiki tano za mazungumzo magumu, serikali ya Israel imeidhinisha, Jumatano, Novemba 22, makubaliano ya kuachiliwa kwa mateka hamsini ili kubadilishana na kuachiliwa kwa wafungwa wa Kipalestina na usitishwaji wa mapigano kwa siku nne katika Ukanda wa Gaza.

Mwanamke akiwa mbele ya bango lenye picha za mateka, huko Ramat Gan, Novemba 22, 2023 baada ya kukamilika kwa makubaliano kati ya Israel na Hamas.
Mwanamke akiwa mbele ya bango lenye picha za mateka, huko Ramat Gan, Novemba 22, 2023 baada ya kukamilika kwa makubaliano kati ya Israel na Hamas. AP - Oded Balilty
Matangazo ya kibiashara

■ Serikali ya Israel iliidhinisha, usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano, makubaliano ya kuachiliwa kwa mateka 50 - wanawake na watoto - walio mikononi mwa Hamas ili kubadilishana na kuachiliwa kwa wafungwa wa Kipalestina na kusitishwa kwa mapiganao kwa siku nne huko Gaza, kulingana na taarifa rasmi. "Serikali ya Israel, jeshi la Israel na vikosi vya usalama vitaendeleza vita kuwarudisha watu wote waliotekwa nyara, kuwaondoa Hamas na kuhakikisha kuwa hakuna tishio zaidi kwa taifa la Israel kutoka Gaza," inaongeza taarifa kwa vyombo vya habari.

■ Umoja wa Ulaya (EU) umeidhinishai kuendelea na misaada yake ya maendeleo kwa Wapalestina.

■ Wafanyakazi 108 wa UNRWA, shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi wa Kipalestina, waliuawa huko Gaza. Madaktari watatu pia walipoteza maisha katika shambulio katika hospitali ya Al-Awda, kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, shirika la Madaktari Wasio na Mipaka, MSF, limesema.

■ Idadi ya vifo kutokana na mashambulizi ya Israel katika Ukanda wa Gaza imefikia vifo 14,128 tangu kuanza kwa vita Oktoba 7, ikiwa ni pamoja na watoto 5,840, kulingana na Wizara ya Afya ya Hamas, madarakani katika eneo hilo la Palestina. Tangu wakati huo, zaidi ya Waisraeli 1,200 wameuawa. Jeshi la Israel limeripoti watu 239 wanaoshikiliwa mateka na kundi la wanamgambo a Hamas.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.