Pata taarifa kuu

Benjamin Netanyahu: 'Hatutasimamisha vita baada ya kusitishwa kwa mapigano'

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameapa kuwa hatositisha vita dhidi ya kundi la wanamgambo wa Hamas katika Ukanda wa Gaza, wakati vita kati ya jeshi la Israel na wanamgambo wa kundi hili vikiendelea kupamba moto katika maeneo mbalimbali ya Ukanda wa Gaza.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamn Netanyahu amesema nchi yake itaedelea na vita dhidi ya Hamas.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamn Netanyahu amesema nchi yake itaedelea na vita dhidi ya Hamas. © Abir Sultan / AP
Matangazo ya kibiashara

"Hatutasimamisha usitishaji mapigano," Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu amesema mwanzoni mwa mkutano wa serikali juu ya kuachiliwa kwa mateka wanaoshikiliwa na Hamas, ambao ulifanyika baada ya mikutano ya serikali na maafisa mbalimbali wa ngazi ya juu jeshini na katika idara ya usalama, linaripoti Gazeti la Israel la Haaretz.

Waziri wa Ulinzi Benny Gantz pia amezungumza katika ufunguzi wa mkutano huo, akisema muhtasari mpana wa mpango huo "ni ngumu na chungu kwa mtazamo wa kibinadamu, lakini ndio makubaliano sahihi."

Kiongozi wa Hamas Ismail Haniyeh alisema katika taarifa mapema leo: "Tunakaribia kufikia makubaliano juu ya usitishaji vita"

Kwa Kiarabu neno lililotumika katika kauli - "hudna" -linahusishwa na aina isiyo ya kudumu ya kutuliza mapigano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.