Pata taarifa kuu

Israel itachukua 'jukumu zima la usalama', Netanyahu aonya

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema hivi pude Jumatatu usiku kuwa nchi yake itakuwa na "jukumu la jumla la usalama" wa Ukanda wa Gaza kwa muda usiojulikana mara tu vita na Hamas vitakapomalizika. 

Mpalestina akiwa amembeba mikononi mwake mtoto aliyepatikana chini ya vifusi vya jengo lililoharibiwa kufuatia shambulio la anga katika kambi ya wakimbizi ya Khan Younis, kusini mwa Ukanda wa Gaza, Jumatatu, Novemba 6, 2023.
Mpalestina akiwa amembeba mikononi mwake mtoto aliyepatikana chini ya vifusi vya jengo lililoharibiwa kufuatia shambulio la anga katika kambi ya wakimbizi ya Khan Younis, kusini mwa Ukanda wa Gaza, Jumatatu, Novemba 6, 2023. AP - Mohammed Dahman
Matangazo ya kibiashara

"Israel itakuwa, kwa muda usiojulikana, itakuwa na wajibu wa jumla wa usalama," amesema katika mahojiano ya televisheni ya ABC News. "Kwa sababu tumeona kile kinachotokea wakati hatuna hilo." Wakati hatuna jukumu hili la usalama, tunaona mlipuko wa ugaidi wa Hamas kwa kiwango ambacho hatungeweza kufikiria.

Waziri Mkuu wa Israel pia kwa mara nyingine tena amekataa wazo la kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza, bila ya kuachiliwa kwa mateka waliotekwa nyara na kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Hamas kutoka Palestina.

Wakati huo huo mapigano makali yanapamba moto kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, ambapo jeshi la Israel lilidai kuukata sehemu mbili, katikati ya ziara ya kikanda ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken. Mashambulio haya ya mabomu yanaathiri hasa raia, ikiwa ni pamoja na kusini mwa eneo hilo. Washington inatangaza kwamba Joe Biden na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu wamejadili "uwezekano wa kusitishwa kwa mbinu" ya jeshi la Israel katika Ukanda wa Gaza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.