Pata taarifa kuu

Ndugu wa mateka wanaoshikiliwa Gaza wakusanyika mbele ya ofisi ya Waziri Mkuu

Maelfu ya watu wamekusanyika siku ya Jumamosijioni mbele ya ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel mjini Jerusalem. Familia hizi za mateka walioondoka Tel Aviv na ambao waliandamana kwa siku kadhaa, wakiungana na maelfu ya watu wengine, wanadai kuachiliwa mara moja kwa mateka wanaoshikiliwa huko Gaza, anakumbuka mwandishi wetu maalum huko Jerusalem, Murielle Paradon.

Maelfu ya watu, zikiwemo familia za mateka wanaoshikiliwa huko Gaza, wamekusanyika tarehe 18 Novemba mbele ya ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel mjini Jerusalem.
Maelfu ya watu, zikiwemo familia za mateka wanaoshikiliwa huko Gaza, wamekusanyika tarehe 18 Novemba mbele ya ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel mjini Jerusalem. AP - Mahmoud Illean
Matangazo ya kibiashara

Edward anaishi kusini mwa Israeli, amejiunga na maandamano kama ishara ya mshikamano: "Kuna watu wa mrengo kushoto kabisa hapa, watu wa mrengo kulia kabisa, watu wasio na dini, watu wa dini. Na sote tumekuja tukiwa na imani kubwa na hitaji kubwa la kuonyesha kwamba tunajihusisha na wale waliotekwa nyara, na taifa zima. Kuna msemo wa Kiebrania unasema kwamba mtu mmoja anapopigwa, kila mtu anapigwa, wakati mtu anatishiwa kila mtu anatishiwa na sisi sote tunatoka kama kitu kimoja. Sasa serikali inatosha? Nadhani serikali inakabiliwa na shida kubwa na ngumu. Lakini kama ingehitajika kuwaachilia wafungwa wote wa Kipalestina, badala ya mateka wetu wote, nadhani Waisraeli walio wengi wangependelea. Ikiwa tunaweza kuwaachilia mateka wetu, wacha tulipe bei ya juu. Wachukueni wafungwa wenu, wafungueni wetu. Na tutaendelea kupambana. "

Familia za mateka pia zimepokelewa jioni na baraza la kiita la Israeli huko Tel Aviv.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.