Pata taarifa kuu

Tanzania yatangaza kifo cha mwanafunzi aliyetekwa nyara na Hamas

Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania imetangaza kifo cha mmoja wa raia wake wawili, mwanafunzi mwenye umri wa miaka 22, aliyechukuliwa mateka na Hamas wakati wa mashambulizi mabaya ya Oktoba 7 dhidi ya Israel. 

Baadhi ya mateka 240 waliotekwa nyara wakati wa shambulizi la Oktoba 7 bado wanazuiliwa katika eneo la Palestina.
Baadhi ya mateka 240 waliotekwa nyara wakati wa shambulizi la Oktoba 7 bado wanazuiliwa katika eneo la Palestina. AP - Leo Correa
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Israel iliwatambua Watanzania wawili, Clémence Félix Mtenga (miaka 22) na Joshua Loitu Mollel (miaka 21) miongoni mwa watu zaidi ya 200 waliotekwa nyara wakati wa shambulio baya lililoanzishwa nakundi la wapiganaji wa Palestina la Hamas, ambalo lilianzisha vita na Israel. Vijana hao wawili walikuwa nchini Israeli kama sehemu ya programu ya mafunzo ya kilimo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Israeli ilisema kwenye X (zamani ikiitwa Twitter) mnamo Oktoba 29.

"Ni kwa masikitiko makubwa tunathibitisha kifo cha Clémence Félix Mtenga," ilisema Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania katika taarifa iliyochapishwa Ijumaa jioni, bila kutaja mazingira ya kifo chake. Wizara hiyo iliongeza kuwa familia yake imefahamishwa na hatua zimechukuliwa kuandaa kurejeshwa kwa mwili wake. "Pia tunapenda kuutaarifu umma kuwa Joshua bado hajulikani aliko," kiliongeza chanzo hicho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.