Pata taarifa kuu

Hamas inaishutumu Israel kwa 'kuchelewesha' kuachiliwa kwa mateka

Mapigano kati ya jeshi la Israel na wapiganaji wa Hamas yamejikita katikati mwa Mji wa Gaza, kaskazini mwa eneo hilo, hasa karibu na baadhi ya hospitali zinazoshukiwa na jeshi la Israel kuwa linahifadhi miundombinu ya Hamas, ambayo inatumia wakazi kama "ngao halisi za kibinadamu", jeshi al Israel linasema.

Moshi ukiongezeka kutoka Gaza baada ya mapigano kati ya Hamas na jeshi la Israel, Novemba 13, 2023.
Moshi ukiongezeka kutoka Gaza baada ya mapigano kati ya Hamas na jeshi la Israel, Novemba 13, 2023. © RONEN ZVULUN / REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Taarifa Muhimu:

►Hamas "imepoteza udhibiti huko Gaza" na wapiganaji wake "wanakimbia kuelekea kusini", Waziri wa Ulinzi wa Israeli Yoav Gallant alisema siku ya Jumatatu baada ya zaidi ya wiki tano za vita na kundi la wapiganaji wa Hamas kutoka Palestina.

►Saa 48 pekee zimesalia kabla ya shughuli za kibinadamu za UNRWA kusitishwa, alitangaza mkurugenzi wake Thomas White siku ya Jumatatu. Kufikia wakati huo, akiba yao ya mafuta itakuwa imekwisha. Israeli bado inakataa kuruhusu mafuta kuingia kupitia kivuko cha Rafah, kwenye mpaka wa kusini wa eneo hilo.

► Waziri Mkuu wa Palestina Mohammed Shtayyeh ametoa wito kwa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya Jumatatu hii "kudondosha misaada" kwa ndege katika Ukanda wa Gaza kusaidia raia walionaswa katika vita kati ya Israel na Hamas.

► Umoja wa Mataifa umetoa rambi rambi kwa wasaidizi wake zaidi ya 100 waliouawa huko Gaza. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres aliameomba kusalia kimya kwa dakika moja saa 9:30 asubuhi kwa saa za ndani katika maeneo ambayo shirika hilo lina uwakilishi.

► Siku ya Jumatatu saa moja usiku Wizara ya Afya ya Hamas kutoka Palestina ilitangaza kwamba idadi ya waliofariki kutokana na mashambulizi ya anga ya Israel katika Ukanda wa Gaza imefikia vifo 11,240 tangu kuanza kwa vita Oktoba 7, wakiwemo watoto 4,630. Tangu tarehe hiyo, zaidi ya Waisraeli 1,200 wameuawa, baada ya mamlaka nchini Israel kurekebisha idadi ya vifo siku Ijumaa, Novemba 10. Jeshi la Israel limeripoti watu 239 wanaoshikiliwa mateka na Hamas.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.