Pata taarifa kuu

Hospitali mbili zasitisha shughuli zao kaskazini mwa Gaza

Hospitali kuu mbili kaskazini mwa Ukanda wa Gaza zimelazimika kufunga milango yao kwa wagonjwa wapya siku ya Jumapili, kulingana na shirika la habarila Reuters. Wafanyakazi wanasema mashambulizi ya Israel na ukosefu wa mafuta na dawa ni hatari na vinaweza kusababisha vifo vya watu ambao tayari wanatibiwa katika hospitali hizo.

Watoto wachanga walitakiwa kuwekwa kwenye mashine za kuongeza joto kwenye vyumba vya kulelea watoto waliozaliwa na uzito pungufu wamewekwa katika vitanda vya kawaida kutokana na kukatika kwa umeme katika hospitali ya al-Shifa, Novemba 12, 2023.
Watoto wachanga walitakiwa kuwekwa kwenye mashine za kuongeza joto kwenye vyumba vya kulelea watoto waliozaliwa na uzito pungufu wamewekwa katika vitanda vya kawaida kutokana na kukatika kwa umeme katika hospitali ya al-Shifa, Novemba 12, 2023. © OBTAINED BY REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Hospitali kaskazini mwa eneo la Palestina zimezuiwa na vikosi vya Israeli na haziwezi kuwatibu wagonjwa, kulingana na wafanyakazi wa matibabu. Israel inasema inakabiliana na wapiganaji wa Hamas katika eneo hilo na kwamba hospitali zinapaswa kuhamishwa. Hospitali kubwa zaidi ya Gaza, Al-Shifa, na kituo kingine kikubwa, Al Quds, zote zilitangaza kuwa zinasitisha shughuli zao siku ya Jumapili.

Daktari wa upasuaji katika Hospitali ya Al-Shifa amesema kulipuliwa kwa jengo kulikuwepo mashine za kuongeza joto kwenye vyumba vya kulelea watoto waliozaliwa na uzito pungufu  kulilazimisha timu za madaktari kuwaweka watoto njiti kwenye vitanda vya kawaida, kwa kutumia nishati kidogo inayopatikana kuendesha kiyoyozi ili kuwapa joto.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.