Pata taarifa kuu

Gaza: Jeshi la Israel aingia katika hospitali ya Al-Shifa

Jeshi la Israel liliingia katika hospitali ya Al-Shifa, ambayo ni kubwa zaidi katika Ukanda wa Gaza, siku ya Jumatano, llikilenga kile linachosema kama kituo cha kimkakati cha Hamas kilichowekwa katika hospitali hii ambapo maelfu ya Wapalestina wanaokimbia vita wamekimbilia.

Wanajeshi wa jeshi la Israel wakiwa kwenye operesheni katika hospitali ya Al-Shifa, Gaza, Novemba 15, 2023.
Wanajeshi wa jeshi la Israel wakiwa kwenye operesheni katika hospitali ya Al-Shifa, Gaza, Novemba 15, 2023. via REUTERS - Israel Defense Forces
Matangazo ya kibiashara

Jengo hilo kubwa la hospitali, kwa siku kadhaa limekuwa kitovu cha mapigano kati ya wanajeshi wa Israeli na wapiganaji wa Kiislamu, ni lengo kuu la Israeli, ambayo imeapa "kuangamiza" Hamas, iliyo madarakani katika Ukanda wa Gaza, tangu shambulio la umwagaji damu lililopotekelezwa na kundi la wanamgambo wa Kipalestina wa Hamas kwenye ardhi yake tarehe 7 Oktoba.

Mapema Jumatano asubuhi, makumi ya wanajeshi wa Israel, wengine wakiwa wamejifunika nyuso zao na kufyatua risasi hewani, walivamia hospitali hiyo iliyoko katika mji wa Gaza, na kuwaamuru watu waliokuemo kujisalimisha, kwa mujibu wa mwandishi wa habari anayefanya kazi na sirika la habari la AFP katika eneo hilo.

"Vijana wote walio na umri wa miaka 16 na zaidi, inueni mikono yenu hewani na tokeni nje ya majengo kuelekea ua wa ndani ili kujisalimisha," walipaza sauti kwa Kiarabu. Israel ilitangaza kuwa inatekeleza "operesheni iliyolengwa na ya usahihi dhidi ya Hamas katika sekta maalum ya hospitali ya Al-Shifa", iliyoko kaskazini mwa Ukanda wa Gaza.

Vifaru katika hospitali

Askari waliwahoji watu katika hospitali hiyo, wakiwemo wagonjwa na madaktari, pia wakifanya msako kwa wanawake na watoto waliokuwa wakilia. Vifaru vya Israel, vilivyokuwa vimeizunguka hospitali hiyo kwa siku kadhaa, viliingia ndani ya jengo hilo, vikiwa vimekaa mbele ya idara mbalimbali ikiwemo chumba cha dharura. Misururu ya Wapalestina, mikono ikiwa juu, ilikusanyika kwenye ua wa hospitali hiyo, huku kwenye korido, wanajeshi wakifyatua risasi hewani huku wakipita chumba hadi chumba, wakionekana kuwatafuta wapiganaji wa Hamas.

Takriban watu 2,300 kulingana na Umoja wa Mataifa, wakiwemo wagonjwa, walezi na watu waliokimbia makazi yao kutokana na vita wako ndani ya al-Chifa katika hali mbaya, bila maji wala umeme. Madaktari na mashirika yasiyo ya kiserikali ya kimataifa yanasema kuwa hakuna hata mmoja wao anayeweza kutoka nje. Vita hivyo vilichochewa Oktoba 7 na shambulio la Hamas katika ardhi ya Israel kwa kiwango kikubwa na ghasia ambazo hazijaonekana tangu kuundwa kwa Israel mwaka 1948.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.