Pata taarifa kuu

Gaza: Operesheni ya jeshi la Israel yaaendelea katika hospitali ya Al-Shifa

Jeshi la Israel linaendelea na operesheni yake Alhamisi hii, Novemba 16, katika hospitali kuu ya Gaza, eneo la kimkakati la kijeshi la Hamas kwa mujibu wa jeshi hilo. Maelfu ya raia wamejazana mahali hapa, na kusababisha wasiwasi mkubwa na huku wana harakati wengi na viongozi mbalimali wakiendelea kukosoa uvamizi huo wa jrshi la Israel katika hospitali hii.

Photo diffusée par l'armée israélienne le 15 novembre 2023 qui montre un soldat se tenant à l'extérieur de l'hôpital al-Chifa.
Picha iliyotolewa na jeshi la Israel mnamo Novemba 15, 2023 inaonyesha mwanajeshi akiwa amesimama nje ya hospitali ya Al-Shifa. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Unachotakiwa kufahamu:

► Jeshi la Israel limekuwa likifanya operesheni "iliyolengwa" katika hospitali ya Al-Shifa, hospitali kubwa zaidi huko Gaza, tangu Jumanne jioni, Novemba 14.

► Jumatano jioni, Israel ilidai kupata "silaha na vifaa vya kijeshi" katika hospitali ya Al-Shifa, jambo ambalo Hamas imekanusha.

►Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limevunja ukimya kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa vita kati ya Israel na Hamas, na kutoa wito wa "kusitishwa kwa mapigano kwa ajili ya kufikisha misaada kwa walengwa na kutenga eneo salama" katika Ukanda wa Gaza. Azimio lililotayarishwa na Malta, lililopitishwa kwa kura 12 za kuunga mkono na tatu zilizopinga (Marekani, Uingereza, Urusi), "linataka usitishaji mkubwa na wa haraka wa mapigano na eneo la kiusalama kwa siku za kutosha."

►Jeshi la Israel lilitangaza kuwa limechukua udhibiti wa majengo ya serikali, likiwemo Bunge, kutoka kwa kundi la wanamgambo la Hamas katika mji wa Gaza.

►Siku ya Jumatano Wizara ya Afya ya Hamas ilitangaza kwamba idadi ya waliofariki kutokana na mashambulizi ya Israel katika Ukanda wa Gaza imefikia vifo 11,500 tangu kuanza kwa vita Oktoba 7, wakiwemo watoto 4,710. Tangu tarehe hiyo, zaidi ya Waisraeli 1,200 kulingana na mamlaka nchini Israel. Jeshi la Israel limeripoti watu 239 wanashikiliwa mateka na Hamas.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.