Pata taarifa kuu

Hamas imepoteza udhibiti wa kaskazini mwa Gaza kulingana na Israel, raia 50,000 wakimbilia kusini

Jeshi la Israel sasa linaendesha operesheni zake katikati mwa mji wa Gaza, kaskazini mwa ardhi ya Palestina ambapo hali ya mamia ya maelfu ya raia bado iko inazidi kuwa mbaya baada ya mwezi mmoja wa vita vibaya.

Wanajeshi wa Israel wakitembea kwenye vifusi huko Gaza, baada ya kutangaza kuwa Hamas imepoteza udhibiti wa eneo la kaskazini mwa eneo hilo, Novemba 8, 2023.
Wanajeshi wa Israel wakitembea kwenye vifusi huko Gaza, baada ya kutangaza kuwa Hamas imepoteza udhibiti wa eneo la kaskazini mwa eneo hilo, Novemba 8, 2023. © RONEN ZVULUN / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Unachotakiwa kufahamu:

► “Wale wanaotoa wito wa usitishaji mapigano mara moja wana wajibu wa kueleza jinsi ya kurekebisha matokeo yasiyokubalika ambayo yanaweza kutokea. Hamas imesalia eneo hili, ikiwa na zaidi ya mateka 200, wakiwa na uwezo na nia ya kurudi kutekeleza yale yaliyotokea Oktoba 7, tena na tena na tena,” Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alisema wakati wa mkutano na vyombo vya habari uliyofanyika siku ya Jumatano katika mkutano wa G7 hukoTokyo, kulingana na Gazeti la Guardian.

► Jeshi la Israel limesema hivi punde Jumatano usiku kwamba Hamas imepoteza udhibiti wa kaskazini mwa Gaza, wakati maelfu ya wakaazi wameondoka eneo hilo kuelekea kusini mwa eneo la Palestina, amesema msemaji wa eneo la Palestina.Jeshi la Israel, Daniel Hagari.

► Qatar inaendesha upatanishi "kwa uratibu na Marekani (...) ili  kuachiliwa kwa mateka 10 hadi 15 kwa kubadilishana na kusitishwa kwa mapigano kwa siku moja hadi mbili", chanzo karibu na majadiliano kimeliambia shirika la habari la AFP. Ni mateka 12, nusu yao wakiwa Wamarekani badala ya "siku tatu za usitishaji wa mapigano".

► Benyamin Netanyahu amerudia kwamba hakutakuwa na usitishaji vita au mafuta yaliyoidhinishwa huko Gaza hadi Hamas iwaachilie mateka 240 inayowashikilia. Waziri Mkuu pia alionya Hezbollah ya Lebanon kwamba itafanya "kosa la maisha yake" ikiwa itajiunga na mzozo ulioanzishwa na Hamas. Israeli inakubali tu kuzingatia uwezekano wa "kusitisha vita kwa muda".

► Wizara ya Afya ya Hamas ya Palestina ilitangaza kwamba idadi ya waliofariki kutokana na mashambulizi ya Israel katika Ukanda wa Gaza imefikia vifo zaidi ya 10,569 tangu kuanza kwa vita Oktoba 7, ikiwa ni pamoja na watoto zaidi ya 4,324. Tangu tarehe hiyo, zaidi ya Waisraeli 1,400 wameuawa, wakiwemo wanajeshi 341, na jeshi la Israel linaripoti watu 240 wanaoshikiliwa mateka na Hamas.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.