Pata taarifa kuu

Marekani: Biden atoa wito wa 'kuongeza misaada kwa kasi na haraka Gaza'

Rais wa Marekani Joe Biden ametoa wito siku ya Jumapili, Oktoba 29,  wa kuongeza ka kasi na haraka misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza, kufuatia upanuzi wa operesheni za kijeshi za Israeli kukabiliana na mashambulizi ya Hamas wiki tatu zilizopita. 

Rais wa Marekani Joe Biden amekuwa akiionya Iran dhidi ya kuisaidia kijeshi Hamas.
Rais wa Marekani Joe Biden amekuwa akiionya Iran dhidi ya kuisaidia kijeshi Hamas. via REUTERS - POOL
Matangazo ya kibiashara

"Rais amesisitiza haja ya mara moja na kwa kiasi kikubwa kuongeza misaada ya kibinadamu ili kukidhi mahitaji ya raia huko Gaza", ameyasema hayo kwa simu akimwambia Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, kulingana na taarifa ya White House.

Amefanya vivyo hivyo katikawito tofauti kwa rais wa Misri Abdel Fattah al-Sissi, chanzo hicho  kimesema.

Wakati huo huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesisitiza wito wake wa kusitisha mapigano mara moja huko Gaza na kuachiliwa kwa mateka waliotekwa na Hamas.

Akizungumza wakati wa ziara yake nchini Nepal, alirudia ombi lake la "kusitishwa mara moja kwa mapigano ya kibinadamu, kuachiliwa bila masharti kwa mateka wote, na utoaji wa misaada endelevu ya kibinadamu kwa kiwango ambacho kinakidhi mahitaji ya watu wa Gaza".

Pia alielezea tena "kulaani kwake kabisa kwa mashambulizi ya kutisha" yaliyofanywa na Hamas tarehe 7 Oktoba, na kuwasilisha salamu zake za rambirambi kwa familia za wanafunzi kumi wa Nepal waliouawa katika shambulio hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.