Pata taarifa kuu

Gaza: Hamas yaweka masharti ya kuachiliwa kwa mateka waliotekwa nyara Oktoba 7

Tawi la kijeshi la Hamas limesema liko tayari, Jumamosi hii, Oktoba 28, kuwaachilia mateka liliowateka nyara wakati wa shambulio lake katika ardhi ya Israel. Kwa Kwa kufanya hivo linaomba kuachiliwa kwa Wapalestina wote wanaozuiliwa nchini Israeli.

Kitengo cha wanajeshi wa Israel kinaonekana kikiwa karibu na mpaka wa Israel na Gaza, Jumamosi, Oktoba 28, 2023.
Kitengo cha wanajeshi wa Israel kinaonekana kikiwa karibu na mpaka wa Israel na Gaza, Jumamosi, Oktoba 28, 2023. © Tsafrir Abayov / AP
Matangazo ya kibiashara

 

"Kwa kuwaachilia huru mateka adui, ambao wako mikononi mwetu ni kuwaondoa wafungwa wote wa Kipalestina katika jela," msemaji wa jeshi la Hamas Abu Obeida amesema katika rekodi ya video.

"Ikiwa adui anataka kufunga kesi hii ya wafungwa kwa mpigo mmoja, tuko tayari kufanya hivyo. Ikiwa anataka mchakato wa hatua kwa hatua, sisi tuko tayari pia,” ameongeza. Kiongozi wa Hamas katika Ukanda wa Gaza, Yahya Sinouar, pia amesema yuko tayari "mara moja" kuhitimisha mabadilishano ya mateka ambao kundi lake linawashikilia kwa sharti ya "kuwafungua wafungwa wote wa Kipalestina" wanaoshikiliwa na Israel.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, ambaye amekutana na familia za mateka siku ya Jumamosi, amwaahidi kwamba Israeli "itatumia njia zote" ili kuhakikisha mateka wote wanaachiliwa.

Watu 9 wa Ufaransa bado hawajulikani walipo

Kwa mujibu wa ripoti ya hivi punde ya mamlaka ya Israel, karibu mateka 230 waliotekwa nyara wakati wa shambulio la Oktoba 7 wanashikiliwa katika Ukanda wa Gaza, eneo la Wapalestina lililo mikononi mwa Hamas.

Watu tisa wa Ufaransa bado hawajulikani walipo, kwa mujibu wa ripoti ya hivi punde iliyothibitishwa na Waziri wa Mambo ya Nje a Ufaransa Catherine Colonna siku ya Ijumaa. Miongoni mwao, kadhaa walichukuliwa mateka.

Zaidi ya watu 1,400 wameuawa nchini Israel tangu shambulio hili la kiwango kikubwa lililotekelezwa na makomando wa Hamas, kulingana na mamlaka ya Israel.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.